• HABARI MPYA

    Wednesday, April 15, 2015

    AZAM FC SARE YA TATU MFULULIZO, 0-0 NA MGAMBO MKWAKWANI, MTIBWA YAICHAPA 1-0 PRISONS MANUNGU

    Na Mwandishi Wetu, TANGA
    AZAM FC imezidi kujitoa katika mbio za ubingwa baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Hiyo inakuwa sare ya tatu mfululizo kwa mabingwa hao watetezi, baada ya awali kutoka 1-1 na Mbeya City Chamazi na 1-1 tena Mtibwa Sugar Manungu.
    Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 39, baada ya kucheza mechi 21 na kuendelea kukamata nafasi ya pili, nyuma ya Yanga SC yenye pointi 46 za mechi 21 pia.
    Simba SC inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake 35 za mechi 21, wakati Kagera Sugae yenye pointi 31 baada ya kucheza mechi 22 ni ya nne.
    Mchezo wa leo Uwanja wa Mkwakwani ulikuwa mkali na kilichoonekana kuiathiri Azam FC ni kucheza mchezo wa kijihami zaidi- ingawa hata hali ya uwanja ilikuwa kikwazo.
    Azam FC imezidi kujitoa kwenye mbio za ubingwa baada ya sare ya 0-0 na Mgambo JKT leo 

    Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Shukrani kwake, Nahodha Shaaban Nditi aliyefunga bao hilo pekee kwa penalti baada ya Mussa Hassan Mgosi kuchezewa rafu na Luagano Mwangama.    
    Kikosi cha Mgambo JKT kilikuwa; Godson Mmasa, Bashiru Chanacha, Abuu Iddi, Ramadhani Malima, Salum Kipanga, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Ally Nassor, Fully Maganga, Malimi Busungu na Salim Gila.
    Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Serge Wawa, Kipee Bolou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Gaudence Mwaikimba, Didier Kavumbagu na Brian Majwega.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC SARE YA TATU MFULULIZO, 0-0 NA MGAMBO MKWAKWANI, MTIBWA YAICHAPA 1-0 PRISONS MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top