• HABARI MPYA

    Saturday, January 11, 2014

    MSIBA MSIBA, MSIBA… KIONGOZI TASWA AAGA DUNIA

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    MWEKA Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na timu ya soka ya chama hicho, Sultan Sikilo amefariki dunia usiku huu katika hospitli ya Rufaa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
    Katibu wa TASWA, Amir Mhando ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba, Sikilo alifikishwa hospitali ya Muhimbili, ambako umauti uimfika akitokea hospitali ya Temeke, Dar es Salaam, Alhamisi wiki hii.
    Pumzika kwa amani sahiba; Sultan Sikilo wa kwanza kulia

    “Ndugu yetu aligundulika ana matatizo ya homa ya ini siku ya Alhamisi katika hospitali ya Temeke na akahamishiwa Muhimbili, ambako umauti umemfika,”amesema Mhando.
    Mhando amesema msiba wa marehemu upo nyumbani kwa wazazi wake Mbagala Maji Matitu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Saa 9:00 Alasiri eneo la Kibada, Kigambni, Dar es Salaam. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSIBA MSIBA, MSIBA… KIONGOZI TASWA AAGA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top