• HABARI MPYA

    Monday, December 09, 2013

    YANGA WAMPA RUHUSA MAALUM KIIZA, LAKINI NANI MTANI JEMBE ATAKUWEPO

    Na Mahmoud Zubeiry, Mombasa
    MUSSA Katabaro, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga SC, amesema amepata taarifa za Hamisi Kiiza kufiwa na baba yake na pamoja na kumpa ‘pole’ wamemruhusu kurejea Uganda kwenye msiba.
    Hamisi Kiiza kulia anarejea Uganda kwenye msiba, kabla ya kujiunga na Yanga kwa maandalizi ya pambano na Simba SC

    Baada ya Uganda kutolewa na Tanzania Bara katika Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, Kiiza alitakiwa kwenda Dar es Salaam kuungana na wenzake walio mazoezini kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba wa Nani Mtani Jembe, wiki mbili zijazo.
    Lakini kutokana na kufiwa na baba yake, mdogo mjini Kampala, Katabaro aliyekuwa Mombasa wakati Bara inaitoa Uganda, alisema; “Kiiza ametoa taarifa za msiba na tumemruhusu kurejea Uganda, akimaliza msiba atakuja Dar es Salaam,”alisema.
    Katabaro wa pili kushoto akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu' kulia kwake 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAMPA RUHUSA MAALUM KIIZA, LAKINI NANI MTANI JEMBE ATAKUWEPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top