| Mfano wa kuigwa; Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' kulia ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya shirikisho hilo, akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Moses Katabaro kushoto wakishangilia ushindi wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars dhidi ya Uganda, The Cranes katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa juzi. Stars ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 na sasa itamenyana na Kenya kesho saa 7:00 mchana katika Nusu Fainali, Uwanja wa Kenyatta, Machakos. |
0 comments:
Post a Comment