| Kila la heri mwana; Mrisho Ngassa alikutana na Diamond Plutinumz jana jioni kwenye Ndege wakati timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ikisafiri kutoka Mombasa kwenda Nairobi, tayari kwa mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya wenyeji, Kenya Jumanne Uwanja wa Kenyatta, Machakos. Stars ilicheza na Uganda juzi, The Cranes Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa na kuitoa kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90, wakati Diamond alifanya onyesho usiku wa siku hiyo ufukwe wa Big Tree Resort, Mombasa na kupagawisha ile mbaya. Wawili hao ni marafiki na wamewahi kufanya tangazo la biashara pamoja. Diamond alimtakia kila la heri Ngassa na Stars katika mchezo wao wa Jumanne na akasema angeweza kubaki, lakini tayari ana mikataba ya maonyesho mengine Dar es Salaam kuanzia jana Coco Beach. |
0 comments:
Post a Comment