• HABARI MPYA

    Tuesday, December 10, 2013

    MECHI YA STARS NA KENYA YAAHIRISHWA, UWANJA WA MACHAKOS HAUFAI, NI MAJARUBA YA MPUNGA

    Na Mahmoud Zubeiry, Machakos
    MECHI ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kati ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ iliyopangwa kuanza Saa 7:00 mchana huu Uwanja wa Kenyatta, Machakos, imeahirishwa na sasa itachezwa Saa 12:00 jioni Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
    Hii ndiyo hali halisi ya Uwanja wa Kenyatta, Machakos

    Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amesema kwamba sababu ya kufikia hatua hiyo ni hali mbaya ya Uwanja wa Kenyatta kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo.
    Makocha wa timu zote, Kim Poulsen wa Tanzania Bara na Adel Amrouche wa Kenya wamekagua Uwanja na kujiridhisha haufai kuchezewa, ingawa Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) alikuwa anashinikiza mechi hiyo ichezwe hapo hapo.
    Lakini pamoja na Musonye kutoa uamuzi huo,  Nyamweya amewaamuru wafanyakazi wa Uwanja wachote maji uwanjani aking’ang’aniza mechi ichezwe hapo.
    Amrouche kushoto akimbishia Nyamweya mbele ya Musonye

    Kim Poulsen ameweka msimamo hachezi Kenyatta


    Musonye akiwapa taarifa rasmi kocha Kim na Mkuu wa Msafara wa Stars, Msafiri Mgoyi kwamba mechi ni Nairobi


    Hatuingizi timu mtaalamu mwenzangu hapa; Amrouche kushoto akizungumza na Kim
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA STARS NA KENYA YAAHIRISHWA, UWANJA WA MACHAKOS HAUFAI, NI MAJARUBA YA MPUNGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top