• HABARI MPYA

    Tuesday, December 10, 2013

    STARS NA HARAMBEE SASA ‘FIFTY FIFTY’ KUCHEZWA LEO AU KESHO…HATA NAIROBI NAKO MVUA INANYESHA ILE MBAYA

    Na Mahmoud Zubeiry, Machakos
    TIMU zote mbili, Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ tayari zimewasili Nairobi kutokea Machakos, kufuatia kuahirishwa kwa mechi baina yao ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge hadi saa 12:00 jioni kutoka Saa 7:00 mchana.
    Timu hizo zimerejea hoteli na zinatarajiwa kuingia Uwanja wa Nyayo, Nairobi kuanzia Saa 11:00 kuanza kupasha misuli moto kwa ajili ya mechi hiyo. Tayari Nusu Fainali nyingine kati ya Zambia na Sudan inaendelea Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa.
    Wachezaji wa Stars, Himid Mao na Mbwana Samatta kulia wakiwa kwenye basi kurejea Nairobi.

    Kevin Yondan na Mrisho Ngassa kulia

    Thomas Ulimwengu kulia

    Lakini bahati mbaya zaidi, hata Nairobi nako kuna mvua kubwa- maana yake mustakabali wa mechi baina ya Kenya na Tanzania Bara bado tata.
    Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye alichukua hatua ya kuuhamishia mchezo huo Nyayo na kusogeza muda mbele, kwa sababu ya hali mbaya ya Uwanja wa Kenyatta, Machakos kufuatia mvua kubwa inayonyesha leo.
    Makocha wa timu zote, Kim Poulsen wa Tanzania Bara na Adel Amrouche wa Kenya waliukagua Uwanja na kujiridhisha haufai kuchezewa, ingawa Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya alikuwa anashinikiza mechi hiyo ichezwe hapo hapo.

    Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mkenya Boniphace Ambani akimsalimia Athumani Iddi 'Chuji' Machakos. Amani amestaafu soka na sasa anafanya biashara Kenya

    Salum Abubakar 'Sure Boy' kulia na Erasto Nyoni

    Ivo Mapunda akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Tanzania, Crezecensia Tryphone  

    Chuji anampa pasi ndefu Ngassa, Ngassa anakimbiza, anapiga krosi, Ambani anafunga....

    Supa Staa; Walimbwende walimfuata Ngassa Machakos na kusahau uzalendo

    Ngassa na Kevin Yondan wakipanga mipango

    Na wakati timu zinajiandaa kwa safari ya kurejea Nairobi kujiandaa na mchezo huo saa 12:00 jioni, Nyamweya aliwaamuru wafanyakazi wa Uwanja wachote maji uwanjani aking’ang’aniza mechi ichezwe hapo.
    Walinzi getini walizuia gari za timu kutoka katika jitihada za kushinikiza mechi ichezwe, lakini hata hivyo CECAFA ilitumia nguvu na mageti yakafunguliwa timu zikatoka kuelekea Nairobi.
    Kwa sasa mvua inanyesha karibu Kenya yote na hata kufikiria mechi hiyo kuiahirisha pengine mvua ya leo inaweza kuwa nafuu kuliko itakayonyesha kesho. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS NA HARAMBEE SASA ‘FIFTY FIFTY’ KUCHEZWA LEO AU KESHO…HATA NAIROBI NAKO MVUA INANYESHA ILE MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top