• HABARI MPYA

    Sunday, December 08, 2013

    BALAA, ARSENAL YAPEWA SPURS RAUNDI YA TATU KOMBE LA FA, RATIBA NZIMA NI NOMA KWA VIGOGO

    KLABU ya Arsenal imepangwa na wapinzani wao wa London Kaskazini, Tottenham katika Raundi ya Tatu yaKombe la FA.
    Manchester City watasafiri kuifuata Blackburn Rovers, Chelsea watamenyana na Derby ugenini na Manchester United watakuwa wenyeji wa Swansea.
    Mabingwa wa sasa, Wigan wataanza kampeni zao za kutetea taji kwa kumenyana na Milton Keynes Dons nyumbani.
    Mechi kali; Arsenal itamenyana na Tottenham Uwanja wa Emirates 
    Jubilant: Wigan won the FA Cup last season against all odds by beating Man City in the final
    Wigan ilishinda Kombe la FA msimu uliopita baada ya kuifunga Man City katika fainali

    Aidha, Liverpool itamenyana na Oldham au Mansfield Uwanja wa Anfield, wakati West Brom itacheza na Crystal Palace, Newcastle na Cardiff na Norwich na Fulham. 
    Oldham iliifunga The Reds 3-2 katika Raundi ya Nne mara ya mwisho na watakutana na kikosi cha Brendan Rodgers kama wataitoa Mansfield katika mchezo wao wa marudiano wa Raundi ya Pili.
    Liverpool pia ilikutana na Mansfield katika Raundi ya Tatu msimu uliopita, na Luis Suarez aliiongoza timu yake kushinda 2-1.
    Tricky customer: Luis Suarez helped knock out Mansfield with a handball last season
    Luis Suarez aliisaidia Liverpool kuitoa Mansfield 

    Mara ya mwisho Arsenal kushinda Kombe la FA ilikuwa mwaka 2005, lakini ili kushinda taji hilo tena italazimika kuwafunga wapinzani wake wakuu. 

    RATIBA RAUNDI YA TATU KOMBE LA FA

    Barnsley v Hartlepool/Coventry
    Yeovil v Leyton Orient
    Liverpool v Oldham/Mansfield
    Nottm Forest v West Ham
    Bristol City v Watford
    Southend v Millwall
    Middlesbrough v Hull
    West Brom v Crystal Palace
    Kidderminster v Peterborough
    Doncaster v Stevenage
    Stoke v Leicester
    Southampton v Burnley
    Newcastle v Cardiff
    Rochdale v Leeds
    Wigan v MK Dons.
    Charlton v Wrexham/Oxford.
    Man Utd v Swansea
    Port Vale v Plymouth
    Norwich v Fulham
    Aston Villa v Sheff Utd.
    Macclesfield v Sheff Wed.
    Sunderland v Carlisle.
    Bolton v Blackpool
    Blackburn v Man City
    Everton v QPR
    Brighton v Reading
    Arsenal v Tottenham 
    Birmingham v Bristol Rovers/Crawley
    Grimsby v Huddersfield
    Ipswich v Preston
    Derby v Chelsea
    Bournemouth v Fleetwood/Burton
    Matches to be played over the weekend of January 4-5.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALAA, ARSENAL YAPEWA SPURS RAUNDI YA TATU KOMBE LA FA, RATIBA NZIMA NI NOMA KWA VIGOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top