ARSENAL imepunguzwa kasi katika Ligi Kuu ya England, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Everton Uwanja wa Emirates, London leo.
Kiungo Mesut Ozil alitangulia kuifungia Arsenal dakika ya 80, lakini Gerard Deulofeu aliyetokea benchi akaisawazishia Everton dakika ya 84.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Jenkinson, Koscielny, Mertesacker, Gibbs, Arteta, Wilshere/Rosicky dk68, Ramsey/Flamini dk68, Ozil, Cazorla/Walcott dk68 naGiroud.
Everton: Howard, Coleman, Distin, Jagielka, Oviedo, Pienaar/Osman dk71, Barkley/Naithsmith dk90, Barry, McCarthy, Mirallas/Deulofeu dk79 na Lukaku.
Ozil akishangilia bao lake la dakika ya 80
Limerudi: Gerard Deulofeu akishangilia baada ya kuifungia Everton bao la kusawazisha
Tim Howard akienda chini kuzuia mpira wa Santi Cazorla
Aaron Ramsey alikosa bao la wazi ambalo Tim Howard aliokoa
Ramsey akijaribu bila mafanikio kumfunga kipa Howard



.png)
0 comments:
Post a Comment