• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 24, 2013

  HII NI KULIKO ZOTE ULIZOWAHI KUZIONA ZA WACHEZAJI KUJIRUSHA KUTAFUTA PENALTI ZA CHEE...ILIKUWA KATIKA MECHI YA REAL NA JUVE JANA USIKU

  NI sawa kusema kiungo wa Chile, Arturo Vidal hakuwa na usiku mzuri jana.
  Vidal alikuwa sehemu ya kikosi cha Juventus kilichoendelea na mwanzo mbaya mbaya wa msimu huu baada ya kufungwa 2-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid.
  Na pamoja na hayo, alifanya kituko cha kijinganga sana yeye mwenyewe binafsi kusaka penalti rahisi, baada ya kujirusha kwenye eneo la hatari bila hata kuguswa.

  Penalti refaaa! Vidal alijirusha na kuanguka Uwanja wa Santiago Bernabeu

  Vidal alipoteza mpira yeye mwenyewe akiwa ameingia kwenye eneo la hatari la Real na kupiga nyasi hivyo mpira ukapoteza mwelekeo, naye akajirusha chini kwenye nyasi za Uwanja wa Santiago Bernabeu.
  Wakati mpira unavuka mstari kutoka nje ili ipigwe goal-kick, huku kukiwa hakuna beki jirani naye, Vidal alianza kulalamika kumuomba refa atoe penalti akiwa ameanguka chini.
  Kuyapa uzito madai yake akanyoosha kidole kabisa kumdanganya refa eti amechezewa faulo ba beki wa Madrid aliyekuwa karibu yake. Ni salama kusema alikuwa analetra umagumashi. 
  Mis-hit: Vidal kicks the turf with no defender anywhere near him
  Bahati mbaya: Vidal alipiga nyasi badala ya mpira huku kukiwa hakuna beki wa Real jirani naye
  Airborne: The Chilean begins to lift off the ground
  Aliingia vizuri tu: Kiungo huyo wa Chile alifanikiwa kuingia vizuri kwenye eneo la hatari la Real
  High-flyer: Vidal's dive is now in full swing
  Abaruka: Vidal akijirusha
  Back down to earth: The Juve midfielder prepares to fall flat on the turf
  Anajirusha: Kiungo wa Juve akijiandaa kudondokea kwenye nyasi baada ya kujirusha
  Are you sure? Real's players look confused as Vidal starts pointing his finger
  Una uhakika? Wachezaji wa Real wakionekana kuchanganyikiwa wakati Vidal anawanyooshea kidole

  Juventus haijainda mechi hadi sasa katika Ligi ya Mabingwa msimu huu na inashika nafasi ya tatu katika Kundi B michano hiyo ikiwa imefikia katikati hayua ya makundi, ikizidiwa pointi mbili na Galatasaray wanaoshika nafasi ya pili.
  Ushindi wa vinara wa kundi hilo, Madrid umetokana na mabao ya Cristiano Ronaldo mawili, huku Fernando Llorente akifunga bao pekee la Juve.

  No diving! Sportsmail's campaign to stop players cheating
  LOGO FOR DAILY MAIL SPORTSMAIL CAMPAIGN - 'No diving'.
  Hakuna kujirusha! BIN ZUBEIRY inaunga mkono kampeni za Sportsmail kuwazuia wachezaji kudanganya marefa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HII NI KULIKO ZOTE ULIZOWAHI KUZIONA ZA WACHEZAJI KUJIRUSHA KUTAFUTA PENALTI ZA CHEE...ILIKUWA KATIKA MECHI YA REAL NA JUVE JANA USIKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top