// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGORONGORO YAALIKWA MICHUANO YA ANOCA, KIINGILIO MECHI YA U20 WANAWAKE 1000/- - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGORONGORO YAALIKWA MICHUANO YA ANOCA, KIINGILIO MECHI YA U20 WANAWAKE 1000/- - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, October 22, 2013

  NGORONGORO YAALIKWA MICHUANO YA ANOCA, KIINGILIO MECHI YA U20 WANAWAKE 1000/-

  Na Boniface Wambura, Ilala
  TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes imealikwa kushiriki Olimpiki ya Afrika itakayofanyika Mei mwakani.
  Mpira wa miguu ni kati ya michezo 22 itakayoshindaniwa katika mashindano yatakayofanyika Gaborone, Botswana chini ya Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA).
  Kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC), Tanzania imepewa nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa Afrika kutokana na kuwa na programu nzuri za vijana hasa chini ya umri wa miaka 17.
  Mudathir Yahya wa Azam FC, mmoja wa nyota wanaotarajiwa kuwamo kikosi cha Ngorongoro

  Hiyo itakuwa ni michezo ya Pili ya Afrika kwa Olimpiki ambapo ya Kwanza ilifanyika mwaka 2010 jijini Rabat, Morocco.
  Wakati huo huo; Kiingilio cha chini kwenye mechi ya wanawake chini ya miaka 20 katika ya Tanzania na Msumbiji itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 1,000.
  Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho ni kwa ajili ya viti vya rangi ya kijani, bluu na chungwa. Viingilio vingine ni sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 10,000.
  Timu ya Msumbiji inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Oktoba 23 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya LAM. Msumbiji yenye msafara wa watu 25 itafikia kwenye hoteli ya Sapphire.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO YAALIKWA MICHUANO YA ANOCA, KIINGILIO MECHI YA U20 WANAWAKE 1000/- Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top