• HABARI MPYA

  Tuesday, October 22, 2013

  MADEGA ANAPOOMBA KURA KWA MANJI AWAGARAGAZE KARIA NA NASSIB

  Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga SC, Wakili Imani Omar Madega (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo, Alhaj Yussuf Manji kushoto juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati timu yao ikimenyana na watani wa jadi, Simba SC na kutoa sare ya 3-3. Madega anagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mwishoni mwa wiki Dar es Salaam akichuana na Wallace Karia na Ramadhani Nassib. Klabu za Ligi Kuu pia zinapiga kura katika uchaguzi huo. Je, Manji atampa kura Madega?   

  Jamani naombeni kura yenu; Kulia Clement Sanga, Makamu Mwenyekiti Yanga SC, kushoto Manji na katikati Madega

  Huyu naye ni mpiga kura, Mohamed Nassor wa Kigoma, atampigia Madega?

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MADEGA ANAPOOMBA KURA KWA MANJI AWAGARAGAZE KARIA NA NASSIB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top