• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 25, 2013

  STEWART ASEMA SIMBA NA AZAM JUMATATU 'TEMEA MATE PEMBENI'

  Na Mahmoud Zueiry, Dar es Salaam
  KOCHA wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amesema kwamba mchezo wa Jumatatu dhidi ya Simba SC utakuwa mkali kwa sababu ni wa vita ya kuwania usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Muingereza huyo amesema kwamba Jumatatu atakutana na timu nzuri na iliyo katika hali nzuri kimchezo kwa sasa, Simba SC hivyo itakuwa shughuli pevu.
  Stewart Hall amesema mechi na Simba SC itakuwa balaa

  Hata hivyo, Stewart amesema anashukuru hata yeye timu yake iko vizuri kuelekea mchezo huo hana majeruhi wa kutisha na hakuna mchezaji muhimu atakayekosekana siku hiyo.
  “Nafurahi nitakuwa na kikosi kamili siku hiyo, ni jambo zuri sana na tunaendelea vizuri na maandalizi, tupo kambini tangu Jumatatu na tunafanya mazoezi kama kawaida,”alisema.
  Azam imeweka kambi katika makao yake makuu, Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo, wakati Simba SC wapo Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam.
  Timu hizo zinalingana kwa pointi, 20 kila moja, sawa na Mbeya City, baada ya kucheza mechi 10, ingawa Simba SC wanakaa juu kutokana na wastani wao mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, Azam ya pili.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STEWART ASEMA SIMBA NA AZAM JUMATATU 'TEMEA MATE PEMBENI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top