• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 24, 2013

  KIPA HUYU WA SIMBA NI MDOGO WA UMBO, MKUBWA WA MAMBO

  Na Mahmoud Zubeiry, Tanga
  MASHABIKI wa Simba SC walipatwa hofu baada ya kipa wao kwanza, Mganda Abbel Dhaira kuumia dakika ya 33 na nafasi yake kuchukuliwa na kipa aliyepandishwa kutoka timu ya vijana, Simba B, Abuu Hashimu dakika mbili baadaye.
  Walikuwa kimya wakiamini sasa wanadondosha pointi tatu mbele ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, baada ya kuona kipa anayeingia ana umbo dogo na pia hajawahi kudaka katika Ligi Kuu.
  Mdogo wa umbo; Abuu Hashimu baada ya kumalizia dakika 10 za kipindi cha kwanza

  Lakini kazi aliyoifanya kumalizia dakika 10 tu za kipindi cha kwanza jana, kwa kiasi fulani iliwatuliza nafasi zao mashabiki hao- wakaamini dogo anaweza kulinda vizuri lango.
  Kipindi cha pili ndiyo Coastal walicharuka zaidi kusaka mabao na Hashimu alipata fursa ya kuupambanua zaidi uwezo wake kwa kuokoa vizuri, ikiwemo kupangua mipira ya juu kwa kuruka hewani na kupigiwa makofi.
  Dakika ya 70, Jerry Santo alimjaribu Hashimu kwa shuti la juu, lakini dogo huyo alienda hewani kupangua mpira huo vizuri licha ya ufupi wake.
  Abuu akienda hewani kupangua shuti la Jerry Santo


  Amepangua

  Wakati anaingia kuchukua nafasi ya Dhaira, mashabiki wa Simba walijawa hofu

  Lakini alisimama imara langoni

  Huyu dogo asije kunichomesha; Abbel Dhaira akiwa benchi baada ya kuumia akimshuhudia Abuu Hashimu akilinda lango la Simba vizuri

  Anadaka kama Juma Kaseja

  Bado alitokea vizuri mipira kudaka, aliweza kuwapanga mabeki na kuanzisha mipira haraka ili timu ifanye mashambulizi ikitoka kushambuliwa. Kwa ujumla dogo ameonyesha yeye ni hazina kama si tu kwa klabu hiyo bali hata kwa taifa pia.
  Kwa kiasi kikubwa udakaji wake anamuiga Juma Kaseja, kipa aliyeidakia timu hiyo tangu mwaka 2003 kabla ya kutemwa mwishoni mwa msimu uliopita.
  Abuu ndiye kipa aliyeidakia Simba B hadi ikatwaa Kombe la Banc ABC mwaka jana ikizifunga timu nzuri zilizotumia nyota wake wa Ligi Kuu kama Azam FC na Mtibwa Sugar.
  Lakini pamoja na kupewa nafasi jana, Abuu ni kipa wa tatui Simba SC baada ya Dhaira na Andredw Ntalla aliyesajiliwa msimu huu kwa mamilioni kutoka Kagera Sugar ambaye jana hakuwepo hata benchi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIPA HUYU WA SIMBA NI MDOGO WA UMBO, MKUBWA WA MAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top