• HABARI MPYA

    Sunday, October 27, 2013

    JIKUMBUSHE MAISHA MAGUMU YA MBABE MUHAMMAD ALI BAADA YA KUFUNGIWA NA SERIKALI YA MAREKANI KUPIGANA KWA KUGOMA KUPIGANA VITA DHIDI YA VIETNAM

    ALIZALIWA kama Cassius Clay, lakini anafahamika zaidi kwa jina Kiislamu alilochagua, Muhammad Ali.
    Wakati kuna picha nyingi zikimuonyesha gwiji huyo wa ngumi akiwa ulingoni, ni picha chache sana zinamuonyesha katika miaka ambayo alifungiwa katika mchezo huo kwa kugoma kuingia jeshini kupigana vita dhidi ya Vietnam.
    "Vita ni kinyume cha mafundisho ya Qur'an tukufu,"alisema. "Siwezi kujaribu kukikuka maandiko. Haturuhusiwi kuingia kwenye vita  isipokuwa tu mwa maelekezo yake Allah au Mitume wake. Hatuiingii kwenye vita na Wakristo au yeyote asiyeamini,".
    Alipogoma kufanya hivyo Aprili 28, mwaka 1967, si kwamba alikamatwa tu, bali alipokonywa leseni ya ngumi na kuvumuliwa mataji yote.
    Baadaye Mahakama ya Houston, Texas ilimkuta na hatia, alkini Mahakama Kuu ya Marekani ilifuta maamuzi hayo mwaka 1971 na Ali akawa huru kurejea ulingoni tena.
    Ali hakutumikia kifungo jela, lakini alizuiwa kupiana kati ya mwaka 1967 na 1971.
    Wakati amezuiwa kupigana alitumia muda wake kuzungumzia masuala ya haki katika shule na vyuo vikuu.
    "Nina furaha kwa sababu nipo huru," alisema akizungumza na jarida la Time mwaka 1968. "Nimeweka msimamo ambao watu weusi wote watauchukua muda si mrefu,"alisema.
    Zifuatazo ni picha zinazomuonyesha Ali kati ya tangu 1968, wakati bondia huyo alipofungiwa, lakini akaendelea kuteka hisia za Wamarekani nchini humo. 

    Nje ya ulingo: Muhammad Ali akiwa amepozi nje ya Alvin Theater, New York (sasa Neil Simon Theatre) Oktoba 1968. James Earl Jones alicheza katika picha ya The Great White Hope, kuhusu bondia mweusi Jack Johnson
    Legends meeting: Ali (right) speaks with James Earl Jones (left) who went on to win the Tony Award for Best Actor in a Play for The Great White Hope in 1969
    Magwiji walipokutana: Ali (kulia) akizungumza na James Earl Jones (kushoto) ambaye alishinda tuzo ya Tony kama mwigizaji bora Best katika picha ya The Great White Hope mwaka 1969
    Reflecting: Ali stands in front of a picture taken from the The Great White Hope while attending a performance of the play
    Ali akiwa amesimama katika picha iliyochukuliwa kwenye sinema ya The Great White Hope alipohudhuria onyesho la sinema hiyo
    His playful side: Ali jokes around with friends
    Ali akitaniana na rafiki
    Telling his story: Ali speaks to a crowd of 1,500 students in Los Angeles in February, 1968. He spent much of his time banned from boxing speaking at public events across the nation like this one
    Ali akizungumza na umati wa wanafunzi 1,500 mjini Los Angeles Februari, mwaka 1968. 
    Controversial: Ali gives a press conference at UCLA, saying the separation of the races is a solution to the 'brewing' race problem in America
    Utata: Ali akizungumza na Waandishi wa Habari UCLA
    Adored: Ali appears at San Francisco City Hall on April 27, 1968 to participate in a draft protest. But his speech drew some negative calls in the crowd of 12,500 when he commented again on the Black Muslim belief of separating the races
    Ali alikuwepo katika ukumbi wa San Francisco City Aprili 27, mwaka 1968. Lakini hotuba yake ilizuia kizaazaa mbele ya watu 12,500 alipozungumzia Waislamu weusi 
    Reading in his downtime: At his home in Chicago, Ali is pictured reading 'Message to the Black Man' by Elihad Muhammad, the leader of the Nation of Islam
    Nyumbani kwake Chicago, Ali akiwa amepigwa picha anasoma kitabu cha 'Message to the Black Man' kilichoandikwa na Elihad Muhammad, kiongozi wa Waislamu wa taifa hilo
    Enthused: Ali greets students at the St John's University campus in Queens, New York in May 1968
    Ali akisalimia wanafunzi wa St John's University huko Queens, New York Mei mwaka 1968
    Eye of the tiger: Muhammad Ali stares at a picture of boxer Sonny LIston who he was training to fight at the time
    Jicho la Chui: Muhammad Ali akiangalia picha ya bondia Sonny LIston ambaye alikuwa anajiandaa kupambana naye wakati huo
    Independence Day: The fighter attends a dinner honoring Floyd McKissick (second left), the director of Congress of Racial Equality. The dinner was held in Columbus, Ohio on July 4, 1968
    Siku ya Uhuru: Bondia huyo alihudhuria chakula cha usiku kwa heshima ya Floyd McKissick (wa pili kushoto), huko Columbus, Ohio Julai 4, mwaka 1968.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JIKUMBUSHE MAISHA MAGUMU YA MBABE MUHAMMAD ALI BAADA YA KUFUNGIWA NA SERIKALI YA MAREKANI KUPIGANA KWA KUGOMA KUPIGANA VITA DHIDI YA VIETNAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top