• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 27, 2013

  WEMA SEPETU APATA MSIBA MZITO, BABA YAKE MZAZI AFARIKI DUNIA LEO

  Na Princess Asia, Mikocheni
  STAA wa filamu nchini na Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Isaac Sepetu, amefiwa na baba yake mzazi, Balozi Isaac Abraham Sepetu, aliyefariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni mjini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
  Wema Sepetu (katikati) amefiwa na baba yake mzazi

  Habari zinasema kwamba, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital hiyo akipatiwa matibabu ya magonjwa ya Kiharusi na Kisukari yaliyokuwa yakimsumbua.
  Balozi Isaac Sepetu amefariki akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. Pole Wema, pole familia ya marehemu ndugu na jamaa.
  Balozi Isaac Sepetu wakati akitibiwa TMJ. Picha kutoka Sufiani Mafoto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WEMA SEPETU APATA MSIBA MZITO, BABA YAKE MZAZI AFARIKI DUNIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top