• HABARI MPYA

  Monday, October 28, 2013

  SIMBA SC WAWAFANYA KITU MBAYA YANGA NANI MTANI JEMBE YA JANA ARUSHA NA MWANZA

  Na Ibrahim Kyaruzi, Dar es Salaam
  MASHABIKI wa Simba wamewagaragaza vibaya mashabiki wa Yanga lkatika bonanza la Nani Mtani Jembe lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.  
  Watani hao wa jadi wameshindana katika michezo mbalimbali iliyoandaliwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kupitia kampeni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa nchi nzima kwa muda wa miezi miwili.

  Huko Mwanza bonanza lilianza saa nne asubuhi katika viwanja vya Polisi Mabatini ambapo pambano la soka kati ya mashabiki wa Simba na Yanga ndio lilifungua dimba . Mchezo huo ulikuwa ambao ulikuwa ni wa raundi ya kwanza ulikuwa mkali sana na hadi mwisho Simba waliibuka washindi kwa goli 3 – 0. Baada ya mchezo huo ilifuata mechi ya pili kati ya watani wa jadi wa Benderambili ambapo pia Simba waliibuka kidedea kwa ushindi wa goli 2-1.
  Bonanza hilo lilipambwa na wasanii wengi maarufu wa jijini Mwanza akiwemo MC Mashidonge ambaye alikuwa ni kivutio cha aina yake kwa amashabiki hao.
  Jioni kulikuwa na mechi kali ya watani wa jadi ambayo muda wa kawaida ulipomalizika timu za watani wa jadi zilitoka sare ya 1-1 na ikaamuliwa zipigwe penati. Katika zoezi hilo Mussa Majid golikipa wa Simba alipangua penati moja na kuwafanya Simba waibuke kidedea kwa ushindi wa goli 5-4. Baada ya mechi hiyo kumalizika golikipa huyo ndiye aliibuka mchezaji bora wa mechi na kujishindia safari ya kwenda Dar es salaam kushuhudia mechi ya watani wa jadi itakayofanyika Desemba 14 jijini Dar es salaam kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe.
  Michezo mingine ilikuwa ni pamoja na kucheza fuusball na kuvuta kamba ambapo pia mashabiki wa Simba waliwaburuza vibaya wapinzani wao na kuibuka washindi ambapo walijipatia zawadi mbalimbali.
  Katika shindano hilo Kilimanjaro inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAWAFANYA KITU MBAYA YANGA NANI MTANI JEMBE YA JANA ARUSHA NA MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top