• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 25, 2013

  MSUMBIJI U 20 WATUA KUIKABILI THE TANZANITE

  Na Boniface Wambura, Ilala
  TIMU ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 imewasili nchini leo (Ijumaa, Oktoba 25 mwaka huu) saa 8.45 mchana tayari kwa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania itakayofanyika kesho (Jumamosi).
  Msumbiji imetua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 25 unaohusisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, na kwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya Sapphire.
  Msumbiji ilitarajia jioni hii (saa 11) kufanya mazoezi yake ya kwanza na ya mwisho ikiwa nchini kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mwenyeji wa Wamakonde; Mkurugenzi wa hoteli ya Sapphire Court, ambayo wamefikia Msumbiji, Sheikh Abdulfatah Salim Saleh

  Kwa upande wa The Tanzanite, Kocha Rogasian Kaijage amesema wamejiandaa vizuri na wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo ambayo matokeo yake ndiyo yatakayoamua mikakati yake kwa ajili ya mechi ya marudiano itakuwaje.
  Viingilio kwa mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na rangi ya chungwa. Viingilio vingine ni sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa katika magari maalumu uwanjani.
  Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuiunga mkono The Tanzanite ili iweze kufanya vizuri kwenye mechi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUMBIJI U 20 WATUA KUIKABILI THE TANZANITE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top