• HABARI MPYA

    Tuesday, October 22, 2013

    SIMBA: TANO HAZIRUDI, TATU TUMEZIRUDISHA …YANGA MSHUMAA UNAWAKA, UNAZIMA…

    Na Saidy Mdoe, Kinondoni
    KWA waliokuwa wakitoka uwanja wa Taifa Jumapili jioni kwenye mechi ya Simba na Yanga, walikutana na nyimbo zilizojaa vituko.
    Miongoni mwa nyimbo hizo zilikuwa na maneno kama haya: Tano hazirudi, tatu tumezirudisha …Yanga mshumaa, unawaka unazima.
    Hao walikuwa ni mamia ya mashabiki wa Simba waliokuwa wakikimbia mchakamchaka kurejea makwao huku wakiwa na furaha ya kurejesha mabao watatu ya Yanga.
    Kwanini wafurahie sare? Ni kwa sababu sare yenyewe ilikuwa ni ya aina yake – Haikuwa ya kawaida.
    Wachezaji wa Simba SC wakishangilia sare na Yanga kutoka nyuma kwa maao 3-0 hadi mapumziko na kumaliza mechi kwa 3-3.

    Yanga wanakwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 3 kupitia kwa Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza.
    Lakini haikuwa kuongoza tu, bali ni pamoja na kuwafunika Simba katika kila idara.
    Mpira ulipoanza Yanga wakagonga pasi kama 22, Simba wakipokonya mpira wanapiga pasi mbili kabla Yanga hawajauchukua tena mpira na kuendelea kucheza draft.
    Kwa shabiki mwenye roho ndogo wa Simba angeweza kutoka uwanjani wakati wa mapumziko na kurejea nyumbani kwake – Hakukuwa na dalili hata chembe ya Yanga kuupoteza mchezo ule – Simba walikufa.
    Lakini soka lina maajabu yake, Simba wakafufuka kipindi cha pili na kurejesha bao moja baada ya lingine na hatimaye mpira ukaisha kwa sare ya 3-3 - huzuni kwa Yanga, furaha kwa Simba.
    Yanga waliongoza 3-0, wakamaliza kwa sare ya 3-3

    Yanga wameyataka wenyewe.
    Naam Saluti5 inashawishika kuamini kuwa Yanga waliyataka wenyewe – walidhani mpira ulimalizika kipindi cha kwanza na kwamba kipindi cha pili ilikuwa ni kama wako mazoezini,  wakalegeza.
    Lakini pengine Yanga pia walianza kuwaza bao 5-0 za Simba na kuona sasa wakati wa kulipiza kisasi umewadia.
    Simba walipopata bao la kwanza la mapema ndani ya kipindi cha pili, iliwachanganya wachezaji wa Yanga, wakaona 5-0 haiji tena labda sasa waitafute 6-1 ili kupata uwiano wa 5-0.
    Hali ikawa mbaya zaidi Simba walipopata bao la 2, Yanga wakataharuki, zile gonga zao tamu zikapotea, goli la tatu lilionekana dhahir kuwa liko njiani.
    Saluti5 inaamini kuwa pengine wakati makocha wa Simba wakiwa mbogo na kutoa mawaidha makali wakati wa mapumziko, wachezaji wa Yanga na makocha wao walikuwa wanakunywa maji na kusubiri muda wa kurejea uwanjani.
    Wachezaji wa Yanga hawakuonekana kama waliandaliwa kisaikolojia kulinda magoli yao. Simba wana haki ya kusema Tano hazirudi, tatu zimerudi.
    MAKALA HII METOKA SALUTI 5 NA IMEANDIKWA NA MMILIKI WA TOVUTI HIYO, SAIDY MDOE.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA: TANO HAZIRUDI, TATU TUMEZIRUDISHA …YANGA MSHUMAA UNAWAKA, UNAZIMA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top