• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 31, 2013

  SHABIKI SIMBA AKIMBIZWA TEMEKE HOSPITALI TAABAN, ABDULFATAH WA SAPPHIRE NAYE AKIONA CHA MOTO

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  MWANACHAMA wa Simba wa tawi la Mpira Pesa, Magombeni, Dar es Salaam, Fii Kambi amekimbizwa hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya SImba na Kagera Sugar ya Bukoba. 
  Uwanja wa Taifa leo uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC, kufuatia Kagera Sugar kupata bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za mchezo timu hizo zikitoka 1-1.
  Shabiki wa SImba, Fii Kambi akiwa amelazwa katika Zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa

  Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa viti na kuvitupia uwanjani.
  Mara moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi. Simba ilitangulia kufunga kupitia kwa Amisi Tambwe dakika ya 45.
  Fii anapelekwa kwenye gari akimbizwe hospitali ya Temeke


  Amelazwa

  Anapelekwa hospitali Temeke

  Abdulfatah ameporwa simu ya Sh. Mlioni 1.8

  Kutokana na vurugu hizo mashabiki wengi walijeruhiwa na kupatiwa huduma katika Zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa na wengine waliondoka na maumivu yao. Watu pia waliporwa simu, fedha na vitu mbalimbali vya thamani.
  Miongoni mwa walioporwa ni mmiliki wa hoteli ya Sapphire Court, Abdulfatah Salim Saleh wakati anateremka jukwaani, akaibiwa simu yake aina ya Blackberry Q10, yenye thamani ya Sh. Milioni 1.8.
  “Tunateremka kukawa na tatizo na milango ya kutokea watu wengi mlango mdogo, milango mingine imefungwa, sasa pale watu wengi tu wameibiwa wengine walikuwa wanalia kuibiwa pochi za fedha zina dola,”alisema Abdulfatah.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHABIKI SIMBA AKIMBIZWA TEMEKE HOSPITALI TAABAN, ABDULFATAH WA SAPPHIRE NAYE AKIONA CHA MOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top