• HABARI MPYA

    Monday, October 28, 2013

    RAIS KIKWETE KUKIMBIA RIADHA MBIO ZA UHURU

    Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    FOMU za mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi kuanzia kesho, huku Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kuchukua fomu namba moja.
    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, Rais Kikwete ndiye atakayepewa fomu nambo moja kwa ajili ya kushirikishi mbio hizo.
    Rais Kikwete atakimbia mbio za uhuru

    “Hizi mbio zina maana kubwa mno ndani ya Taifa letu, Rais Jakaya Kikwete muda wote anasisitiza na kupigania amani. Amani ni yetu sote, si vyema kumuachia Rais Kikwete peke yake kuipigania, hivyo yeye ndiye atakayekuwa namba moja katika kuchukua fomu na kushiriki mbio hizo,” alisema.
    Melleck alisema, katika kuhakikisha kila mtu anashiriki kutakuwa na vituo 13 vitakavyofunguliwa kwa ajili ya kutoa fomu hizo, huku pia kukiwa na watu maalumu watakaozisambaza maofisini na hata majumbani.
    Melleck alisema, fomu hizo zitatolewa kwa Sh 100,000 kwa wale watakaotaka kukimbia mbio za kilomita tatu, Sh 2,000 mbio za kilomita tano, Sh 6,000 kwa atakayeshiriki moja kati yam bio za kilomita 21 au 42.
    “Hizi mbio ni muhimu zaidi kwa ajili ya Taifa letu, hivyo ni vyema kwa Watanzania wote wakashiriki ili kuipigania amani iliyopo nchini mwetu.
    “Tunataka kuungana na Rais Kikwete katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kuleta umoja, amani na mshikamano ndani ya Tanzania na ndilo lengu la mbio hizi.
    “Bado tunaendelea kuwaomba wadhamini wajitokeze kuzidhamini, kwani nafasi bado ipo wazi na watambue hata wao ni sehemu ya kupigania amani ya taifa letu,” alisema Melleck.
    Innocent Mellek wa kwanza kushoto katika uchaguzi wa TFF jana

    Katika mbio hizo, zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia mbio za kilomita 3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na Full Marathon yenyewe kilomita 42.
    Mratibu huyo anasema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
    “Hapa tunachotaka kufanya katika mbio za kilomita 3 ni kuwaomba kama vile viongozi maarufu wa dini mbalimbali pamoja na viongozi wetu ili kushiriki, kwa kudumisha amani na upendo.
    “Pia tutahakikisha kama mbio za kilomita 5, zinakuwa kwa ajili ya kuchangia watu wenye mahitaji mbalimbali na tayari tuna uhakika mkubwa wa wanariadha maarufu zaidi duniani kushiriki,” Alisema.
    Melleck alisema, wamejipanga mno ili kuhakikisha wanafanya mambo makubwa zaidi na ambayo yataleta tija kwa taifa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS KIKWETE KUKIMBIA RIADHA MBIO ZA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top