• HABARI MPYA

  Sunday, October 20, 2013

  RAIS KIKWETE KUSHUHUDIA MPAMBANO WA SIMBA NA YANGA LEO

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete huenda akapata fursa ya kushuhudia mchezo wa wapinzani wa jadi, Simba na Yanga leo ambao utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
  Lakini Kikwete hatakwenda Uwanja wa Taifa, bali kama kuutazama mchezo huo itakuwa ni kupitia Azam TV inayoshirikiana na Televisheni ya Taifa, TBC 1 kurusha moja kwa moja matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Rais Kikwete kulia akipokea jezi kutoka kwa Nizar Khalfan wakati anacheza Vancouver Whitecaps ya Canada. Kwa sasa Nizar anachezea Yanga SC.

  Na rais Kikwete ambaye ni mpenzi wa Yanga ataishuhudia mechi hiyo akiwa mkoa mpya wa Njombe ambako amekwenda kwa ziara ya wiki moja tangu juzi, Ijumaa Oktoba 18, 2013.
  Akijibu swali kwa kifupi juu ya uwezekano wa Rais Kikwete kutazama mechi hiyo kwenye Televisheni, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu alisema; “Ndiyo”, baada ya kuulizwa na BIN ZUBEIRY, kwa kuwa sasa Ligi Kuu inaonyeshwa kwenye Televisheni, je Mh Kikwete atapata fursa ya kutazama mechi ya leo?”.
  Simba na Yanga zinashuka dimbani leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara.
  Simba SC iko juu ya Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zao 18, wakati mabingwa watetezi wana pointi 15 na Azam FC wameshikilia kwa pamoja usukani wa ligi hiyo na Mbeya City kwa kila timu kuwa na pointi 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS KIKWETE KUSHUHUDIA MPAMBANO WA SIMBA NA YANGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top