• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 27, 2013

  WAWILI WADAIWA KUKAMATWA NA RUSHWA UCHAGUZI TFF, ZOEZI BADO BICHI KABISA WATER FRONT

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  WAJUMBE wawili wa wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanadaiwa kushikiliwa na Polisi kwa saa kadhaa kwa tuhuma za kukutwa na fedha ambazo zinadaiwa zilitaka kutumika kuwahonga Wajumbe wenzao kwa ajili ya uchaguzi Mkuu unaoendelea hivi sasa ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
  Wajumbe wa TFF wamefikishiwa katika hoteli ya Landmark, Ubungo, Dar es Salaam na waliokamatwa inadaiwa walikamatwa na Polisi jana usiku na kulazwa katika kituo cha Tabata, kabla ya kuachiwa kwa dhamana leo. 
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, wawili kati yao wamekamatwa na rushwa Sh. Milioni 3

  Taarifa zinasema walioakamtwa walikutwa na Sh. Milioni 3 na wamedai walitumwa na wamewataja wagombea waliowatuma na lengo lao.
  Haijajulikana undani haswa wa sakata hilo na juhudi za kuwapata Maofisa wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuzungumzia suala hilo zimeshindikana kwa kuwa leo si siku ya kazi.
  Zoezi la uchaguzi wa TFF bado bichi kabisa likiwa linaendelea kwenye ukumbi wa Water Front na muda huu ndiyo wagombea wa nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wapo katika hatua za mwisho za kujieleza.
  Baada ya hapo, itafuatia nafasi ya Makamu wa Rais, inayohusisha wagombea watatu, Ramadhani Nassib, Walace Karia na Imani Madega na wagombea Urais, Jamal Malinzi na Athumani Nyamlani watamalizia.
  Baada ya kukamilika kwa zoezi la Wajumbe kujieleza ndipo zoezi la kupigwa kura litaanza na wazi kulingana na hali halisi, litaisha usiku wa manane na inaweza kuchukua hadi kesho ili kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAWILI WADAIWA KUKAMATWA NA RUSHWA UCHAGUZI TFF, ZOEZI BADO BICHI KABISA WATER FRONT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top