• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 28, 2013

  EL MAAMRY KUONGOZA BODI YA TFF

  Na Boniface Wambura, Dar  Salaam
  MKUTANO Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umemteua Said Hamad El Maamry kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambayo kazi yake kubwa ni kusimamia mali za shirikisho.
  El Maamry ambaye kitaaluma ni mwanasheria na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati huo ikiwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ataongoza bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe watano.
  Mzee El Maamry kulia akiwa Dk Ramadhani Dau (katikati) na Yussuf Kitumbo kushoto

  Wajumbe wengine wa bodi hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ambaye anakuwa Makamu Mwenyekiti, Dk. Ramadhan Dau, Mohamed Abdulaziz na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EL MAAMRY KUONGOZA BODI YA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top