• HABARI MPYA

  Sunday, October 20, 2013

  MANJI AGONGANA NA HANS POPPE UWANJA WA TAIFA..WAZIRI MAKALA 'AKIONA CHA MOTO' KWA WALINZI WA MAGETI

  Naibu Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla alipata kasheshe baada ya kukutwa geti alilotakiwa kutumia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuona mechi ya Simba na Yanga limefungwa na mwenye ufunguo hayupo. 

  Hata hivyo baada ya jitihada za hapa na pale, kijana aliyekuwa na ufunguo alitokea akamfungulia Mheshimiwa Makala

  Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji kulia akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Abdallah Bin Kleb, katika eneo la VIP A, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

  Tishio la Jiji; Kutoka kulia Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Mussa Katabaro, Abdallaha Bin Kleb na Seif Ahmed 'Magari'

  Mheshimiwa Makala alisalimiana na Manji baada ya kuingia uwanjani

  Kutoka kulia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Joseph Itang'are 'Kinesi' anayemsikiliza Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Said Pamba na kushoto na Meneja wa zamani wa klabu hiyo, Evarist Hagila

  Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' kulia akimuonyesha kitu Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Ibrahim Masoud 'Maestro' na kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto 

  Menyekiti wa Chama cha Soka (Tabora), Yussuf Kitumbo akimsalimia Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, DK Ramadhani Dau, Kulia ni Wakili Said El Maamry 

  Hans Poppe akiingia Uwanja wa Taifa kwa kujiamini kabisa

  Kulia Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uendelezaji wa jengo dogo la Yanga SC liliopo Mtaa wa Mafia, Ridhiwani Kikwete katikati

  Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Mohamed

  Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga akiingia Uwanja wa Taifa na vazi la Wekundu wa Msimbazi

  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen kulia akiwa na kocha wa timu za vijana, Mdenmark mwenzake, Jacob Michelsen

  Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Mfaransa Patrick Liewig akiwa Uwanja wa Taifa leo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANJI AGONGANA NA HANS POPPE UWANJA WA TAIFA..WAZIRI MAKALA 'AKIONA CHA MOTO' KWA WALINZI WA MAGETI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top