• HABARI MPYA

  Jumanne, Oktoba 29, 2013

  MBEYA CITY MWENDO MDUNDO, AZAM HAWANA RAHA KILELENI

  Na Princess Asia, Mbeya
  MBEYA City imezidi kuipumulia Azam FC kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya leo. 
  Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City inayofundishwa na kocha maarufu, Juma Mwambusi itimize pointi 23 baada ya mechi 11, sawa na Azam.
  Mbeya City imeshinda 2-0 leo

  Hata hivyo, Azam wanabaki kileleni kwa kuwa wana wastani mzuri zaidi wa mabao ya kufunga na kufungwa, zaidi ya Mbeya City inayoangukia nafasi ya pili, wakati Yanga SC sasa inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake 22. 
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Mbeya City yamefungwa na Peter Mapunda dakika ya 67 na Deogratius Julius dakika ya 79.
  Katika mechi nyingine za leo, Rhino Rangers imeichapa 1-0, Ruvu Shooting ya Pwani Uwanja wa Ally Hassan, Tabora, bao pekee la Abbas Mohamed dakika ya 71.
  Yanga SC imeichapa 3-0 Mgambo JKT Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora, mabao ya Mbuyu Twite, Hamisi Kiiza na Didier Kavumbangu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY MWENDO MDUNDO, AZAM HAWANA RAHA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top