• HABARI MPYA

  Tuesday, October 29, 2013

  KIIZA SASA BEGA SAWA NA TAMBWE MBIO ZA KIATU CHA DHAHABU LIGI KUU

  Na Princess Asia, Dar es Salaam
  HAMISI Friday Kiiza ‘Diego’ wa Yanga SC leo hii amefikisha mabao nane katika mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kufunga bao moja leo katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Hii inakuwa mechi ya tatu mfululizo Mganda huyo anafunga mabao, kuanzia sare ya 3-3 na wapinzani wa jadi, Simba SC alipofunga mawili na ushindi wa 3-0 dhidi ya Rhino Rangers Uwanja huo huo wa Taifa, Dar es Salaam alipofunga mara mbili pia.
  Hamisi Kiiza sasa ana mabao sawa na Tambwe wa Simba SC

  Kiiza sasa analingana kwa mabao mchezaji aliyekuwa anaongoza, Mrundi, Amisi Tambwe wa Simba SC, ambaye mechi tatu sasa hajafunga bao.  
  Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes anafuatiwa na mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar ambaye pia ana mabao saba.
  Amisi Tambwe mabao yamekauka hadi Kiiza amemkuta

  Wanaofuatia ni mfungaji bora wa msimu uliopita, Kipre Tchetche wa Azam FC mwenye mabao sita sawa na Elias Maguri wa Ruvu Shooting na Themi Felix wa Kagera Sugar, wakati Tumba Swedi wa Ashanti ana mabao matano.

  WANAOONGOZA KWA MABAO LIGI KUU:
  JINA TIMU MABAO
  Amisi Tambwe Simba SC 8
  Hamisi Kiiza Yanga SC 8
  Juma Luizio Mtibwa 7
  Kipre Tchetche Azam FC 6
  Elias Maguri Ruvu Shoot 6
  Themi Felix Kagera 6
  Tumba Swedi Ashanti 5
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIIZA SASA BEGA SAWA NA TAMBWE MBIO ZA KIATU CHA DHAHABU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top