• HABARI MPYA

    Monday, October 28, 2013

    KIM AITA 30 FUTURE YOUNG TAIFA STARS

    Na Boniface Wambura, Ilala
    KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya pili (Future Young Taifa Stars) kitakachoingia kambini Novemba 9 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Chalenji.
    Kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia ya Kenya ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na Kim kwenye kikosi hicho ambacho hukitumia kuangalia uwezo wa wachezaji kabla ya kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
    Kikosi hicho kamili ambacho Novemba 13 kitacheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars kinaundwa na; makipa Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).
    Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen

    Mabeki ni David Luhende (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Himid Mao (Azam), Issa Rashid (Simba), Ismail Gambo (Azam), John Kabanda (Mbeya City), Kessy Khamis (Mtibwa Sugar), Michael Pius (Ruvu Shooting), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Said Moradi (Azam) na Waziri Salum (Azam).
    Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Farid Mussa (Azam), Haruni Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Khamis Mcha (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga), William Lucian (Simba).
    Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hussein Javu (Yanga), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mwagane Yeya (Mbeya City) na Paul Nonga (Mbeya City).
    Kim amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager chenyewe kitaingia kambini Novemba 12 jijini Dar es Salaam ambapo siku inayofuata ndipo kitakapocheza mechi na Future Young Taifa Stars.
    Baada ya mechi hiyo, kambi ya Future Young Taifa Stars itavunjwa wakati Taifa Stars itaondoka Novemba 14 mwaka huu kwenda Arusha ambapo itaweka kambi na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kwenda Nairobi, Kenya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.
    Wachezaji 16 wa kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Novemba 12 mwaka huu kinaundwa na Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).
    Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).
    Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.     
    Wakati huo huo: Mechi kati ya timu ya Taifa ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania (The Tanzanite) dhidi ya Msumbiji lililochezwa juzi (Oktoba 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 6,190,000.
    Washabiki waliohudhuria mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika iliyomalizika kwa The Tanzanite kuibuka na ushindi wa mabao 10-0 walikuwa 5,003. Viingilio vilikuwa sh. 1,000, sh. 2,000, sh. 5,000 na sh. 10,000.
    Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 944,237.29, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,247,900, gharama za mchezo sh. 599,573 wakati wamiliki wa uwanja walipata sh. 449,679.
    Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilipata sh. 149,893 huku Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likipata sh. 1,798,718.
    Mechi ya marudiano kati ya The Tanzanite na Msumbiji itachezwa kati ya Novemba 8 na 10 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIM AITA 30 FUTURE YOUNG TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top