• HABARI MPYA

    Tuesday, October 29, 2013

    ARSENAL KUSAJILI KINDA MNIGERIA MWENYE KIPAJI CHA HATARI, AMEWAFUNGA MANNE PEKE YAKE MEXICO KOMBE LA DUNIA LA VIJANA UAE

    KLABU ya Arsenal inamfuatilia kinda mwenye kipaji Mnigeria, Kelechi Iheanacho baada ya kufunga mabao manne dhidi ya Mexico katika mechi ya Kombe la Dunia la FIFA kwa vijana chini ya umri wa miaka 17. 
    Iheanacho, mwenye umri wa miaka 17, anaongoza kwa mabao kwenye mashindano hayo baada ya kufanya vitu adimu dhidi ya mabingwa wa CONCACEF katika mchezo wa ufunguzi wa makundi.
    Baada ya mechi, aliimbia Fifa.com: "Nimefunga mabao manne katika mechi moja kwenye mechi nyingi tu, lakini ni mitaani napocheza na rafiki zangu. Lakini haijawahi kutokea katika mechi ya kimataifa,".

    Tai mdogo wa dhahabu: Kelechi Iheanacho anaing'arisha Nigeria Kombe la Dunia la 17 UAE
    Arsenal's French manager Arsene Wenger
    Kifaa: Kocha wa Arsene Wenger anaweza kumpata kinda huyo wa Nigeria

    Msaka vipaji Mkuu wa Gunners, Steve Rowley yuko Falme za Kiarabu kuangalia mashindano hayo na inafahamika amevutiwa na kiwango cha kiungo huyo. 
    Arsenal itatakiwa kuhakikisha inamnasa kijana huyo, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa ikiwemo kutoa pasi za mabao manne katika mechi za makundi.
    VIDEO Nenda kaangalie Iheanacho alivyofunga na anavyoshangilia
    Kelechi Iheanacho of Nigeria scores his second goal
    Poa sana: Iheanacho akifunga katikati ya mabeki wa Mexico

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL KUSAJILI KINDA MNIGERIA MWENYE KIPAJI CHA HATARI, AMEWAFUNGA MANNE PEKE YAKE MEXICO KOMBE LA DUNIA LA VIJANA UAE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top