WASHAMBULIAJI Neymar na Robinho walionekana kutaka sana kubadilishana jezi katika mechi baina ya timu zao, AC Milan na Barcelona Ligi ya Mabingwa jana usiku... na wakafanya hivyo wakati wa mapumziko!
Licha ya kuchezea wote timu ya taifa ya Brazil, Robinho anabakia kuwa shujaa mkubwa wa Neymar na wawili hao walibadilishana jezi wakati refa anamaliza kipindi cha kwanza.
Neymar alitoa heshima zake kwa winga wa Milan, anayemzidi miaka nane, kabla ya mchezo wa jana, lakini akamuonyesha kazi uwanjani.
Mapema: Winga wa AC Milan, Robinho na mshambuliaji wa Barcelona, Neymar walibadilishana jezi wakati wa mapumziko jana
Neymar aliposti picha yake akiwa mdogo pamoja na nyota huyo wa zamani wa Man City katika Instagram akisema: "Leo ni siku maalum kwangu...kwa kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya mkali wangu, ambaye nimekuwa nikimfuatilia wakati wote tangu nikiwa mdogo na ni heshima kucheza dhidi yake. Bahati nzuri wakati wote, lakini leo ni Barca hahahah, nakupenda,".
Wachezaji wote walianzia soka yao klabu ya Santos ya Brazil kabla ya kuhamia Ulaya kwa uhamisho wa fedha nyingi.
Robinho alihamia Real Madrid mwaka 2005, akisajiliwa na vigogo hao wa Hispania kwa dau la Pauni Milioni 20 wakati Neymar alitua Barcelona mapema msimu huu kwa pauni Miloni 50.
Miaka hiyo: Neymar ameposti picha yake akiwa na shujaa wake Robinho kwenye Instagram jana
Pozi: Robinho akizungumza na Neymar baada ya mechi ya AC Milan na Barcelona Uwanja wa San Siro
Wakati huo huo, mechi hiyo ya Kundi H iliisha kwa sare ya 1-1. Bahati mbaya kwa Neymar, alimshuhudia Robinho akiwafungia bao la kuongoza The Rossoneri dakika ya 10, baada ya mabaki wa Barca kujichanganya.
Javier Mascherano alichanganyana na beki mwenzake Gerard Pique na Robinho akaunasa mpira kabla ya kugongeana pasi na Mbrazil mwenzake Kaka, kisha akafunga.
Pamoja na hayo, bao la Milan halikudumu sana baada ya Lionel Messi kusawazisha dakika 13 baadaye.
Bao la kuongoza: Robinho alitumia mwanya wa mabeki wa Barcelona kujichanganya kuifungia Milan bao la kuongoza
Mfungaji wa bao: Robinho akishangilia baada ya kuifungia The Rossoneri jana
La kusawazisha: Lionel Messi akimfunga kipa Marco Amelia kuisawazishia Barcelona
Umalizijia mzuri: Messi akipongezwa na wenzake, Wabrazil Dani Alves na Neymar baada ya kufunga
Ignazio Abate akiteleza kuondosha mpira miguuni mwa Neymar
Wacheaji wa Milan akiwemo Mario Balotelli na Sulley Muntari wakiruka kuzuia mpira wa adhabu wa Messi
Nigel De Jong akipambana na Andres Iniesta
Robinho akipambana na Alves kugombea mpira
0 comments:
Post a Comment