• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 28, 2013

  SIMBA SC NA AZAM FC KATIKA PICHA LEO TAIFA...

  Watafunga wengine leo, si wewe; Beki wa Simba SC, Hassan Hatibu akimkwatua mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco 'Adebayor' anayekwenda chini katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam FC ilishinda 2-1.

  Winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga alikaribia kufunga leo kama anavyoonekana hapa akikosa bao la wazi licha ya kufanikiwa kuwatoka mabeki na kumpiga chenga kipa Abbel Dhaira

  Hassan Hatibu akipambana na John Bocco

  John Bocco pia alikosa bao la wazi kufuatia krosi nzuri ya Joseph Kimwaga ambayo alishindwa kuunganisha ikapitiliza

  Issa Rashid 'Baba Ubaya' alimkaba sana Kipre Tchetche pamoja na kufungwa mabao yote ya Azam FC leo

  Mfungaji wa bao la Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' akienda chini baada ya kupamiwa na Humphrey Mieno wa Azam FC

  Betram Mombeki wa Simba SC akipambana na Erasto Nyoni wa Azam

  Zahor Pazi wa Simba akipambana na Humphrey Mieno wa Azam

  KIpre Tchetche akimfunga tela William Lucian 'Gallas'

  Mzee bomoa benki, usajii hapa huna timu; Katibu Mkuu wa zamani wa Simba SC, Kassim Dewji akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kulia 

  Namna watu wanvyofuatilia mchezo kwa umakini, na hii mara nyingi hutokea timu yao inapokuwa imefungwa 

  Farid Mussa naye alikosa bao la wazi baada ya kuingia akitokea benchi 

  Kipre Tchetche akimtoka Baba Ubaya 

  Salum Abubakar 'Sure Boy' alimvisha kanzu saizi yake Amri Kiemba

  Kipa wa Simba SC akidaka mpira juu ya kichwa cha mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco huku mabeki wake wakiwa tayari kumsaidia

  Kikosi cha Azam leo

  Kikosi cha Simba SC leo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA AZAM FC KATIKA PICHA LEO TAIFA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top