// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BRANDTS KUPANGUA KIKOSI YANGA, BARTHEZ NJE KESHO BAADA YA KUFUNGWA MABAO 11 MECHI TISA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BRANDTS KUPANGUA KIKOSI YANGA, BARTHEZ NJE KESHO BAADA YA KUFUNGWA MABAO 11 MECHI TISA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 22, 2013

    BRANDTS KUPANGUA KIKOSI YANGA, BARTHEZ NJE KESHO BAADA YA KUFUNGWA MABAO 11 MECHI TISA

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    KIPA Ally Mustafa ‘Barthez’ anaweza kupumzishwa katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu yake na Rhino Rangers ya Tabora, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika mechi tisa alizodaka Barthez hadi sasa, amefungwa mabao 11 na inaonekana kudaka mfululizo tangu msimu uliopita kunamchosha na bila shaka Deo Munishi ‘Dida’ atasimama langoni kwa mara ya kwanza kesho katika Ligi Kuu tangu asajiliwe na Yanga msimu huu kutoka Azam.
    Kwa ujumla, kocha Mholanzi Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts anatarajiwa kufanya marekebisho makubwa katika safu yake ya ulinzi kesho baada ya matokeo ya sare ya 3-3 na wapinzani wa jadi Simba SC Jumapili, Uwanja wa Taifa, wakitoka kuongoza 3-0 hadi mapumziko.
    Kutoka kulia Frank Domayo, Ally Mustafa 'Barthez', Nizar Khalfan na Athumani Iddi 'Chuji
    Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anaweza kuanzia benchi, wakati Juma Abdul ataenda beki ya kulia kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite, atakayehamia katikati kucheza na Kevin Yondan.
    Kuna uwezekano pia wakongwe Athumani Iddi ‘Chuji’ na Haruna Niyonzima nao wakapumzishwa ili ‘kuweka akili sawa’ baada ya sare isiyotarajiwa mwishoni mwa wiki na Frank Domayo akatengeneza safu ya kiungo kwa pamoja na Salum Telela au Hamisi Thabiti.
    Hayatarijwi mabadiliko yoyote katika safu ya ushambuliaji ya Yanga na bila shaka Brandts ataendelea kuwatumia pamoja pale mbele Mrisho Ngassa, Hamisi Kiiza na Didier Kavumbangu.   
    Brandts alikasirika mno baada ya sare ya juzi na kuwaita wachezaji wake makanjanja (unproffessionals) na ndiyo maana walikubali kutoka kuongoza kwa mabao 3-0 hadi kulazimishwa sare ya 3-3 katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Akizungumza baada ya mchezo huo, beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, aliyerithi mikoba ya Mbelgiji Tom Saintfiet Oktoba mwaka jana, alisema kwamba ni uzembe kutoka kuongoza kwa 3-0 hadi mapumziko na kutoa sare ya tatu.
    Anahitaji kupumzisha mwili; Barthez amekuwa akidaka mfululizo tangu msimu uliopita na wazi inaonekana sasa anahitaji kupumzika. Hili ni bao la tatu la kusawazisha la Simba juzi.

    “Nafikiri sare tuliyopata tumejitakia wenyewe, wakati nimeona kipindi cha kwanza tumecheza vizuri sana, tumepata nafasi nyingi, tulikuwa tayari kiasi cha kutosha. Katika dakika 10 za mwisho tayari mchezo waliokuwa wanacheza wachezaji wangu ungeona ulikuwa wa kijinga, walifanya vitu vya kipumbavu, walikuwa wanacheza kwenye kiungo tu, wanakaa na mipira wanafanya mbinu fulani,”.
    “Kisha nikakasirika sana, tuliporudi vyumbani, wachezaji fulani wakawa wanapayuka, aaah tatu bila, tatu bila, ni ukanjanja sana, hivyo nikawaambia, kama hamtaelekeza akili zenu mchezoni, wanaweza wakafunga  bao moja, la pili na la tatu. Niliwaambia katika chumba cha kubadilishia nguo, waulize wachezaji wangu,”. 
    “Na ndicho kilichotokea kipindi cha pili, wamerudi uwanjani, wakapoteza mwelekeo na Simba SC wakarudisha mabao yote. Haya ni matunda ya kukosa umakini, lakini bado tulipata  nafasi nzuri kipindi cha pili, mwishowe nimesikitishwa sana, kwa sababu ni ukanjanja sana,” alisema.
    Brandts alisema kwamba hali iliyojitokeza jana Uwanja wa Taifa si mara ya kwanza katika timu yake, kwani mara kadhaa makosa kama hayo yamekuwa yakifanyika hata katika mechi zilizopta, ila juzi waliruhusu mabao mengi ambayo ni mbaya kwa timu kama Yanga.
    Brandts alisema lawama ni za wachezaji wote, kwa sababu iliyokuwa inacheza ni timu na akasema angeweza kushinda hata mabao sita iwapo wachezaji wake wangecheza kwa umakini.
    “Huwezi kuzuia kwa asilimia 95, lazima ucheze kwa uangalifu na umakini, kama hutafanya hivyo huwezi kupata matokeo mazuri. Kama walivyocheza kwenye mechi (iliyopita) na Kagera Sugar (Bukoba, Yanga ilishinda 2-1). Wachezaji walicheza kwa uangalifu na umakini,”alisema.
    Brandts alisema katika mazoezi ya timu hiyo kila siku anafanyia kazi kila idara na wazi matokeo ya jana yalitokana na vijana wake kulewa sifa baada ya kuongoza mabao 3-0.
    Pamoja na matokeo hayo, Yanga ikiwa na pointi 16 ndani ya mechi 10 ilizocheza, inazidiwa pointi nne na Azam na Mbeya City zinazoongoza ligi na tatu na Simba SC walio nafasi ya pili, Brandts amesema bado ana matumaini ya kutetea ubingwa.
    “Bado nina matumaini ya kutetea ubingwa, kwa sababu ligi bado mbichi, haiishi wiki ijayo, tunakwenda kufanyia kazi mapungufu yetu baada ya mchezo huu (na Simba SC) na kisha tunaendelea na mapambano kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu,”alisema.
    Hadi mapumziko, tayari Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza mawili, lakini kipindi cha Simba SC ikasawazisha kupitia kwa Betram Mombeki, Joseph Owino na Gilbert Kaze.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRANDTS KUPANGUA KIKOSI YANGA, BARTHEZ NJE KESHO BAADA YA KUFUNGWA MABAO 11 MECHI TISA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top