• HABARI MPYA

  Monday, October 21, 2013

  NYOTA BARCELONA WATUA NADHIFU ILE MBAYA ITALIA KUIKABILI AC MILAN LIGI YA MABINGWA KESHO

  KIKOSI cha Barcelona kimewasili mjini Milan leo kwa maandalizi ya mchezo wa Kundi H wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan wachezaji wake wakiwa wamependeza kwa mavazi yao ya nadhifu.
  Barcelona itameyana na wenyeji wao hao, Milan kwenye Uwanja wa San Siro Jumanne usiku, lakini nyota kama Neymar, Alex Song na Dani Alves walionekana kupendeza zaidi baada ya kutua Italia.
  Wakiwa wamepigilia shati kali, suti za nguvu na miwani ya jua, watatu hao walifunika mbaya kiasi cha kuonekana kama nyota wa filamu wakati kikosi cha timu ya Katalunya kinatua mjini humo.  

  Mastaa wa sinema? Neymar (kushoto), Dani Alves (katikati) na Alex Song (kulia) wakionekana watanashati mjini Milan

  Safari kutoka Barcelona hadi Milan inawakutanisha tena wachezaji wa timu hizo kutokana na timu hizo mbili kuwa zimekutana mara sita katika misimu miwili iliyopita huku Barca wakiongoza kupata matokeo mazuri na kuitoa Milan katika Ligi ya Mabingwa mara mbili.
  Barca inaingia kwenye mchezo wa kesho ikiwa haijapoteza pointi wala kuruhusu hata nyavu zake kuguswa kwenye mechi za Kundi H, lenye timu za Celtic na Ajax pia. 
  Milan kwa sasa wapo katika mwanzo mgumu katika ligi ya kwao, Serie A wakiwa wameachwa kwa pointi 13 na vinara AS Roma.  
  Timu hiyo ya Italia pia inakabiliwa na janga la majeruhi, kipa Christian Abbiati, beki Daniele Bonera na washambuliaji Stephan El Shaarawy, Mario Balotelli na Giampaolo Pazzini wapo katika chumba cha matibabu.
  Double denim: Alexis Sanchez (left) and Jonathan dos Santos (right) show-off their designer shirts
  Alexis Sanchez (kushoto) na Jonathan dos Santos (kulia) 
  On board: Barcelona stars striking a pose on their flight to Milan
  Kwenye ndege: Nyota wa Barcelona wakiwa wamepezi kwenye kuelekea Milan
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOTA BARCELONA WATUA NADHIFU ILE MBAYA ITALIA KUIKABILI AC MILAN LIGI YA MABINGWA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top