// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA WAWABURUZA YANGA NANI MTANI JEMBE, JANGWANI KAMA WAMELALA! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA WAWABURUZA YANGA NANI MTANI JEMBE, JANGWANI KAMA WAMELALA! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, October 22, 2013

  SIMBA WAWABURUZA YANGA NANI MTANI JEMBE, JANGWANI KAMA WAMELALA!

  PAMOJA na mchezo wa watani wa jadi kuisha kwa sare ya 3-3 Jumapili ya wiki iliyopita, Simba wameanza kuongoza katika kampeni ya "Nani Mtani Jembe?" inayoendelea hivi sasa kwa kuwashirikisha mashabiki wa klabu hizi mbili kongwe nchini.
  Mpaka sasa Simba wana kitita cha Shilingi 50,012,500.00 wakati watani wao wa jadi Yanga wana Shilingi 49,987,500.00. Upigaji wa kura katika kampeni hii unahusisha mashabiki kununua Bia ya Kilimanjaro na kusoma namba zilizo chini ya kizibo na kutuma kwa ujumbe wa simu wakianza na jina la timu wanayoishabikia kwenda 15440 na moja kwa moja Shilingi 1,000 kupunguzwa kutoka kwa wapinzani na kuwekwa kwa timu yao. Matokeo ya Nani Mtani Jembe yanapatikana katika tovuti ya http://kilitime.co.tz/campaigns/nmj/
  Kampeni ya "Nani Mtani Jembe?" inaendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa klabu za Yanga na Simba.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WAWABURUZA YANGA NANI MTANI JEMBE, JANGWANI KAMA WAMELALA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top