• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 30, 2013

  TASWA NAO WAMPA HEKO MALINZI KUMBWAGA NYAMLANI

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimetoa pongezi kwa uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliochaguliwa Jumapili iliyopita chini ya rais, Jamal Malinzi aliyemshinda Athumani Nyamlani.
  "Tunaungana na wapenda michezo na Watanzania kwa ujumla kuitakia kila la heri Kamati ya Utendaji ya TFF na shirikisho hilo kwa ujumla chini ya Rais mpya Jamal Malinzi na Makamu wake, Wallace Karia,".
  Jamal Malinzi kulia akikabidhiwa mpira na Rais aliyemaliza muda wake, Leodegar Tenga kushoto

  "TASWA inaamini Malinzi, Karia na wajumbe wao ni wazoefu na ni watu wenye kujua mambo mengi yanayohusu mpira wa miguu nchini, hivyo tunaamini watakuwa viongozi wazuri kwa nafasi zao katika kuhakikisha shirikisho hilo linasonga mbele,".
  "Tunawatakia kila la heri Wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji, huku tukiamini hawatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliowaamini kushika nafasi hizo,".
  "TASWA na waandishi wa habari za michezo kwa ujumla hapa nchini tunaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo,"imesema taarifa ya TASWA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TASWA NAO WAMPA HEKO MALINZI KUMBWAGA NYAMLANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top