• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 26, 2013

  EL CASHICO! KARIBU KATIKA MECHI YA GHARAMA KUBWA ZAIDI (PAUNI MILIONI 417) KUWAHI KUTOKEA DAIMA– BARCELONA WENYEJI WA REAL MADRID NOU CAMP

  KARIBU katika mechi ya gharama kubwa zaidi duniani – wachezaji 22 wa bei mbaya zaidi daima wenye thamani ya Pauni Milioni 417 kuumana uwanjani... Barcelona wanaikaribisha Real Madrid leo Jumamosi katika El Clasico ya kwanza msimu huu: Messi v Ronaldo, Neymar v Bale, Pique v Ramos.
  Huku timu ya Carlo Ancelotti ikizidiwa pointi tatu na kikosi cha Gerardo Martino katika La Liga, kipigo kitatengeneza tofauti kubwa baina ya timu hizo mwanzoni mwa msimu.  
  Katika miaka ya karibuni imekuwa mechi ya mchuano mkali, ufundi, na mabao. 

  Mbele: Barcelona kwa sasa wapo kileleni mwa La Liga, wakiwa wameshinda mechi nane, sare moja katika mechi tisa
  On their toes: Real are in third place, winning seven, drawing one and losing one of their nine
  Wanawafukuzia: Real wapo nafasi ya tatu, wakiwa wameshinda mechi saba, sare moja na kufungwa moja katika mechi tisa
  Barcelona (4-1-2-3)
  Victor Valdes – Akademi
  Alitarajiwa kuondoka Nou Camp msimu huu bada ya Monaco kutoa ofa kubwa ya kumnunua na Pepe Reina akatajwa kuja kuziba pengo lake, lakini kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 amebaki na amedaka mechi saba bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa msimu huu katika mechi 12. 7/10.
  Number one: Valdes (left) has held his spot between the sticks despite offers elsewhere in Europe
  Namba 1: Valdes (kushoto) ni kipa anayeheshimika Ulaya

  Dani Alves - Pauni Milioni 23
  Bila shaka ndiye beki bora zaidi wa kulia duniani. Anafahamika zaidi kwa shughuli yake uwanjani, akipanda kusaidia mashambulizi na kuzuia kwa ustadi mkubwa. 9
  Masterful: Like Marcelo for Real, Alves is as astute going forward as he is defending
  Mtaalamu: Kama Marcelo wa Real, Alves anapanda  kushuka

  Gerard Pique - Pauni Milioni 5
  Katika kitabu chake binafsi, Sir Alex Ferguson amemtaja beki huyo wa kati mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4 kwamba bora katika kutoa pasi na anahamasisha ushindi. Anasifika na kuheshimika sana awapo uwanjani popote. 9
  Bargain: Pique was signed back from Manchester United for just £5million
  Beki mstaarabu: Pique alisajiliwa tena kutoka Manchester United kwa Pauni Milioni 5

  Carles Puyol - Akademi
  Akiwa na umri wa miaka 35 anaweza kuonekana mzee, lakini sentahafu huyo aliyeichezea mechi 100 Hispania bado ana mengiya kufanya, kwa ujumla katika mechi za wapinzani hao wa Hispania. Ni mzoefu na anajua kuongoza vyemka jahazi la timu yake. 8
  Mr Barcelona: He's 35-years-old, but his experience of El Clasico's should shine through
  Mr Barcelona: Ana umri wa miaka 35, lakini uzoefu wa Puyol ni muhimu katika El Clasicos 

  Adriano - Pauni Milioni 8.1
  Akiwa amepunguziwa mshahara kwa pauni 77, Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 28 anafahamika kama ‘Utility Man’ na tovuti ya Barca. Beki wa kushoto chaguo la kwanza aliyefunga mabao mawili msimu huu. 7
  Full-blooded: Another attacking full-back, Adriano can be hot and cold down the wing
  Mpiganaji: Beki mwingine anayeshambulia sana, Adriano atakimbiza sana kwenye winga yake leo

  Sergio Busquets – Akademi
  Ana kila sababu ya kuitwa mchezaji mkubwa baada ya mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo huo. Kiungo huyo tegemeo wa Barcelona ana Medali za Dhahabu za Kombe la Dunia, Ubingwa wa Ulaya na Kombe la Ulaya. 9
  The dirty work: Busquets is described by some as Barcelona's most important midfielder
  Mtu wa kazi: Busquets ni kiungo muhimu Barca

  Xavi – Akademi
  Mtaalamu wa tiki-taka akiwa na Medali za kutosha bado ni mtu muhimu ndani ya Barca hususan katika mechi kama hizi. Akiwa na umri wa miaka 33 bado anaonekana yuko vizuri na hana dalili za kuchuja hata kesho. 9
  Central man: Xavi's brain shows no sign of slowing down on the pitch after years at the very top
  Mtu wa kazi: Akili ya Xavi kimchezo inamaanisha yeye no bora sana

  Andres Iniesta – Akademi
  Pacha huyo wa Xavi katikati ya Uwanja akiwa anazidiwa miaka minne na mwebnzake huyo, anaweza kuchukua maukumu mara mkongwe huyo atakapoondoka. Ni mtaalamu wa kutengeneza mabao.  9
  Brother in arms: Xavi's parralel man, Iniesta has more playing time ahead of him
  Kaka wa kambo: Mtu wa kulia wa Xavi, Iniesta ana muda zaidi wa kucheza Barca

  Alexis Sanchez - Pauni Milioni 22
  Winga huyo wa Chile alifahamika duniani baada ya Kombe la Dunia mwaka 2010. Bado hajafikia haswa ubora ule wa Barca, lakini anaweza kucheza katika timu hiyo. 8
  Winger: Sanchez needs a big match on the highest level for Barca, and that could come on Saturday
  Winga: Sanchez anahitaji mechi zaidi ili kulata uzoefu na kufikia ubora wa Barca

  Neymar - Pauni Milioni 48.6
  Hatimaye ametua Barca msimu huu kuunda safu ya ushambuliaji na mkali mwenzake kutoka Amerika Kusini, Messi. Akiwa amefunga mabao mawili tu hadi sasa, atapenda kuweka kumbukumbu zake katika mechi yake ya kwanza wapinzani hao kucheza. 9
  Big money: Neymar has settled in quickly at the Nou Camp after Barcelona splashed out on the Brazilian
  Mchezaji ghali: Neymar amezoea haraka Nou Camp baada ya kununuliwa kwa Pauni Milioni na Barcelona kutoka Santos ya Brazil

  Lionel Messi – Akademi
  Nini zaidi unaweza kusema? Hizi ni baadhi ya takwim: Amefunga mabao 18 na kutoa pasi za mabao 11 katika mechi 25 zilizopita za El Clasicos. Huwa mtu mwingine kabisa anapocheza dhidi ya Madrid. 10
  Say no more: Messi loves playing against Madrid, and has 18 goals in El Clasicos
  Hakuna cha kusema zaidi: Messi anapedna kucheza dhidi ya Madrid, na amefunga mabao 18 katika El Clasicos

  JUMLA YA GHARAMA: Pauni Milioni 106.7. 
  VIWANGO KWA UJUMLA: 94/110
  Real Madrid (4-2-3-1)
  Diego Lopez - Pauni Miloni 3
  Alianza kupewa nafasi na Jose Mourinho badala ya Iker Casillas na Ancelotti amefuata utaratibu huo. Kipa huyo hodari mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 ni mahiri mno kuokoa michomo. 8/10
  Ahead of the game: Lopez has overtaken Real legend Iker Casillas as the club's main goalkeeper
  Kuelekea mechi: Lopez amempindua gwiji wa Real, Iker Casillas kuwa kipa wa kwanza klabu hiyo

  Alvaro Arbeloa - Pauni Milioni 5
  Ni chaguo la kwanza katika beki ya kulia tangu arejee mwaka 2009 katika klabu hiyo aliyojiunga nayo awali akiwa kinda. Beki huyo wa zamani wa Liverpool ni nguzo imara katika safu ya ulinzi ya Real. 7
  Solid: The reliable right-back has been a regular feature at the club in the past few years
  Kisiki: Beki hodari wa kulia aliyeishika beki ya kulia kwa miaka michache iliyopita

  Sergio Ramos - Pauni Milioni 23
  Beki asiye na mambo mengi ambaye anatulia na mpira hakika bado ni mtu muhimu katika klabu hiyo. Katika msimu wake wa tisa Bernabeu ni mtu mwenye uzito ndani ya chumba cha kubadilishia nguo cha Real. 9
  Mainstay: Ramos brings calmness to the group, and is in his ninth season at the club
  Mtu mzima: Ramos anaunganisha na kuleta umoja ndani ya kikosi, na ana misimu tisa katika klabu hiyo

  Raphael Varane - Pauni Milioni 8.5
  Beki wa kati mwenye ufundi wa hali ya juu, alijihakikishia namba kikosi cha kwanza baada ya kucheza vizuri kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa, Real ikiifunga Manchester City msimu uliopita. Akiwa ana umri wa miaka 20, anaweza kuja kuwa beki wa kati tegemeo wa Madrid miaka ijayo. 8
  Youth on his side: At just 20-years-old, Varane (right) could be a future great at the Bernabeu
  Kinda hatari: Akiwa na umri wa miaka 20, Varane (kulia) anaweza kuwa tegemeo la Bernabeu baadaye

  Marcelo - Pauni Milioni 5.4
  Mbrazil huyo anashambulia zaidi katika beki ya kushoto, ingawa pia anafanya vizuri kazi yake ya ulinzi na ana uzoefu sasa wa mechi za wapinzani. 8
  Bright: Marcelo can be an attacking option as well as a solid left-back, and brings excitement down the flanks
  Safi: Marcelo anashambulia zaidi

  Asier Illarramendi - Pauni Milioni 34
  Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa dau la kiwango cha kati, akiwa ana umri wa miaka 23 ameonyesha ni kiungo hodari mkabaji aliyesajiliwa kutoka Real Sociedad msimu huu na ameingia kwenye kikosi cha kutokana na Xabi Alonso kuwa majeruhi, lakini amedhihirisha ubora wake. 8
  Pressure: lllarramendi cost Madrid £34million from Real Sociedad in the summer
  Presha: lllarramendi aliigharimu Madrid Pauni Milioni 34 kutoka Real Sociedad msimu huu

  Sami Khedira - Pauni Milioni 12
  Huyu ni tegemeo la safu ya kiungo ya Madrid. Anaichezesha timu vizuri na kuvunja mashambulizi ya timu pinzani. Unaweza kumuita kiungo mmoja bora ambaye anaifanya Real iwe imara. 8
  Strong: Khedira keeps things ticking over, and is just as important as any other in the Real midfield
  Mashine: Khedira anaiongoza vyema safu ya kiungo ya Real 

  Gareth Bale - Pauni Milioni 86
  Akiwa amefunga mwanzoni, lakini mchezaji huyo ghali duniani amekuwa na mwanzo mgumu Real kutokana na kuandamwa na majeruhi yanayomuweka nje ya kikosi cha timu hiyo kwa muda mrefu. Yuko tayari kucheza  El Clasico yake ya kwanza. 9
  Building up: Bale has had a stop-start opening to his Real career, but the Nou Camp could bring the best of him
  Anajipanga: Bale amekuwa na mwanzo mgumu Real, lakini anatarajiwa kucheza leo Nou Camp

  Isco - Pauni Milioni 23
  Moja ya sababu za Mesut Ozil kuondoka katika klabu hiyo, Mchezaji huyo namba 10 wa Hispania alikataa ofa ya Manchester City ili kujiunga na timu hiyo msimu huu. Ameanza na moto akiwa amefunga mabao mabao matano katika mechi sita. 8
  Bagged: Isco was targeted by several of the world's richest clubs in the summer, but Real got their man
  Hiki kifaa: Isco alitakiwa na klabu kadhaa tajiri na kubwa duniani msim huu, lakini akachagua

  Cristiano Ronaldo - Pauni Milioni 80
  Ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao katika mechi sita mfululizo za El Clasicos. Amefunga mabao 18 katika mechi 14 za klabu na timu yake ya taifa msimu huu. 10
  The man: Ronaldo seems to have been on the form of his life for the last three years
  Mkali kweli: Ronaldo inaelezwa yupo katika kiwango cha juu zaidi maishani mwake katika miaka mitatu iliyopita

  Karim Benzema - Pauni Milioni 30
  Mshambuliaji wa kati wa Real asiyepinka kwa sasa baada ya Gonzalo Higuain kuondoka, lakini akiwa amefunga mabao manne katika mechi 11 msimu huu anaweza kuanza ili adhihirishe makali yake na kuisaidia timu leo. 8
  Up top: Benzema (left) is now Real's first choice centre-forward after battling it out with Higuain last term
  Mtu wa juu: Benzema (kushoto) sasa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Real baada ya kuondoka kwa Higuain msimu uliopita
  JUMLA YA GHARAMA: Pauni Milioni 309.9m
  VIWANGO KWA UJUMLA: 91/110
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EL CASHICO! KARIBU KATIKA MECHI YA GHARAMA KUBWA ZAIDI (PAUNI MILIONI 417) KUWAHI KUTOKEA DAIMA– BARCELONA WENYEJI WA REAL MADRID NOU CAMP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top