• HABARI MPYA

  Thursday, September 12, 2019

  AZAM TV YAONGEZA MIKATABA YA KURUSHA MICHUANO YA ASFC NA MECHI ZA TAIFA STARS ‘LIVE’

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesaini mkataba wa miaka minne na kampuni ya Azam Media Limited kwa ajili ya kuonyesha moja kwa moja mechi za Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars pamoja na mashindano ya Kombe la shirikisho hilo, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Mkataba wa awali wa Azam Sports umefikia tamati msimu uliopita na sasa pande hizo zimesaini mkataba mpya wa miaka minne wenye thamani ya shilingi bilioni 4.5.
  Pia mkataba wa kuonesha mechi za Taifa Stars umegharimu shilingi milioni 400 ambazo ni sawa shilingi milioni 100 kwa mwaka, na kwenye kila mechi Taifa Stars itapata shilingi milioni 35 kutoka Azam Media.

  Akitoa ufafanuzi wa mkataba huo Mkuruguenzi wa Michezo wa Azam Media Patrick Kahemele amesema mechi za Taifa Stars zilizodhamini na Azam ni zile za kirafiki zitakazokuwa kwenye kalenda ya FIFA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM TV YAONGEZA MIKATABA YA KURUSHA MICHUANO YA ASFC NA MECHI ZA TAIFA STARS ‘LIVE’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top