• HABARI MPYA

    Monday, March 13, 2017

    ZAMBIA WALIVYOTAMBA MICHUANO YA AFRIKA U-20

    PAMOJA na Zambia kutwaa ubingwa wa Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, pia imetawala katika tuzo za michuano hiyo.
    Zambia ndio mabingwa wapya wa U-20 Afrika baada ya kuifunga Senegal 2-0 jana mjini Lusaka - na shukrani kwa wafungaji wa mabao hayo, Patson Daka na Edward Chilufyakipindi cha kwanza.
    Mbali ya kuwa timu ya pili ya Kusini mwa Afrika baada ya Angola mwaka 2001 kutwaa taji hilo, Zambia pia wanakuwa wenyeji wanne wa michuano hiyo kutwaa Kombe hilo baada ya Morocco mwaka 1997, Ghana mwaka 1999 na Kongo mwaka 2007.
    Zambia ilikuwa timu pekee kushinda mechi zote kwenye mashindano hayo na kutwaa taji hilo kibabe katika ardhi ya nyumbani.
    Ikicheza mbele ya umati wa mashabiki 50,000 waliofurika Uwanja wa Taifa wa Lusaka, akiwemo Rais wa nchi hiyo, Edgar Lungu, 'Chipolopolo Wadogo' waliwafurahisha Wazambia.  
    Guinea imefanikiwa kukamata nafasi ya tatu ya mashindano hayo, baada ya kuifunga Afrika Kusini mabao 2-1 jana katika mchezo uliotangulia. 
    Patson Daka amekuwa mchezaji Bora wa Mashindano, wakati Mchezaji Bora wa mechi ya Fainali amekuwa Mangani Banda wa Zambia pia.
    Nyota wa Afrika Kusini, Luther Singh ndiye amekuwa mfungaji bora kwa mabao yake manne, sawa na Edward Chilufya na Patson Daka wa Zambia.
    Fashion Junior Sakala wa Zambia amefunga mabao matatu, akifuatiwa na Liam Jordan wa Afrika Kusini, Eric Ayuk Mbu (Cameroon), Morlaye Sylla (Guinea) na Ousseynou Diagne wa Senegal waliomaliza na mabao mawili kila mmoja.  
    Waliomaliza na bao moja kila mmoja ni; Tercious Malepe (Afrika Kusini), Samuel Gouet, Kalvin Jih Ketu, Olivier Mbaizo (Cameroon), Mostafa Abdalla, Karim Hassan, Nasser Maher (Misri), Naby Bangoura, Mohamed Aly Camara, Yamodou Touré (Guinea), Abdoul Karim Danté, Moussa Diakite, Sékou Koita (Mali), Aliou Badji, Krepin Diatta, Ibrahima Niane (Senegal), Hassan Hassan, Walaa Mohamed (Sudan), Emmanuel Banda na Enock Mwepu (Zambia)
    Aidha, kikosi Bora cha CAF kinaundwa na kipa; Mangani Banda wa Zambia, mabeki; Ousseynou Diagne (Senegal), Mamadou Mbaye (Senegal) na Solomon Sakala (Zambia)
    Viungo: Krepin Diatta (Senegal), Ibrahima Niane (Senegal), Sylla Morlaye (Guinea), Edward Chilufya (Zambia) na Fashion Sakala (Zambia)
    Washambuliaji ni Luther Singh wa Afrika Kusini, Patson Daka wa Zambia. Wachezaji wa akiba ni 
    Lamine Sarr wa Senegal, Prosper Chilufya (Zambia), Enock Mwepu wa Zambia, Grant Margeman wa Afrika Kusini, Liam Jordan wa Afrika Kusini, Yamodou Toure wa Guinea, Mohamed Aly Camara wa Guinea.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMBIA WALIVYOTAMBA MICHUANO YA AFRIKA U-20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top