• HABARI MPYA

  Wednesday, March 08, 2017

  MECHI YA YANGA NA ZANACO KURUSHWA AZAM TV

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Zanaco ya Zambia utarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Azam.
  Yanga wamewauzia Azam TV haki za matangazo ya mchezo huo utakaofanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na maana yake hiyo ni faraja kwa mashabiki wa timu hiyo ambao hawataweza kwenda uwanjani, hususan wa nje ya Dar es Salaam.
  Yanga iliingia 32 Bora Ligi ya Mabingwa baada ya kuitoa Ngaya Club de Mde katika hatua ya mchujo

  Yanga inaingia kambini leo kwa maandalizi ya mchezo huo baada ua jana kufanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushindi wa 6-1 dhidi ya Kiluvya United ya Pwani katika mchezo wa kukamilisha hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo inayojulikana pia kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana, mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa alifunga mabao manne peke yake, huku mengine yakifungwa na viungo Geoffrey Mwashiuya na Juma Mahadhi. 
  Yanga sasa itamenyana na Prisons katika Robo Fainali Machi 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Robo fainali nyingine zitakuwa kati ya Simba SC na Madini FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Azam FC na Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kagera Sugar na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Kaitaba.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA YANGA NA ZANACO KURUSHWA AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top