• HABARI MPYA

  Sunday, April 17, 2016

  SABABU TATU LAZIMA IIADABISHE TOTO LEO TAIFA

  Na Renatha Msungu, DAR ES SALAAM
  KUNA sababu tatu ambazo zinafanya Simba wapambane waifunge Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.  
  Moja; Simba SC inamenyana na Toto Africans leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa inahitaji pointi ili kujiweka sawa katika mbio za ubingwa.
  Mbili; Imekwishaanza kuaminika Toto ni timu kiboko ya Simba, hivyo leo Wekundu wa Msimbazi wanatakiwa kufuta imani hiyo.
  Na tatu; Toto ni tawi la Yanga pale Mwanza, mahasimu wa jadi wa Simba. Yanga imeifunga Simba mechi zote mbili za Ligi Kuu msimu huu, hivyo leo ikikubali kufungwa na mtoto wa mtani wao, aibu yake watajifungia chumbani.  
  Mashabiki wa Simba wataweka wapi sura zao wakifungwa na Toto leo?

  Na ikitoka kutolewa katika Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kufungwa 2-1 na Coastal Union ya Tanga mapema wiki hii, Simba SCinahitaji kuwapoza machungu mashabiki wake kwa kuitandika Coastal leo.
  Kocha Mkuu wa Simba, Mganda Jackson Mayanja amesema kikosi chao kinapaswa kuachana na mawazo ya kupoteza nafasi ya Kombe la TFF, na badala yake waelekeze nguvu zao katika mechi za Ligi Kuu ili waweze kufanya vizuri
  katika mchezo wa leo.
  Mayanja Amesema kinachopaswa kwa wachezaji ni kujituma uwanjani, ikiwemo nidhamu ya mazoezi, jambo litakalowasaidia kufanya vizuri katika Ligi Kuu.
  Amesema ana matumaini mchezo huo utakuwa mgumu, kwa sababu wapinzani wao nao wamejipanga kupata pointi tatu muhimu ili waweze kujiweka nafasi nzuri katika Ligi Kuu msimu huu.
  Simba inaendelea kuongoza Ligi baada ya kufikisha pointi 57 baada ya kucheza mechi 24, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56 za mechi 23 huku Azam wakiwa na pointi 55 namechi 24 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SABABU TATU LAZIMA IIADABISHE TOTO LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top