• HABARI MPYA

    Sunday, October 04, 2015

    NGASSA AJENGA HESHIMA ‘SAUZI’, AFANYA MAMBO BALAA FREE STATE YASHINDA 1-0, BIDVEST WITS ‘WAKOLEA’ KWA MRISHO

    NAAM. Sasa Afrika Kusini wanajua kuna mchezaji anaitwa Mrisho Khalfan Ngassa (pichani kushoto) yuko Bethelehem na mashabiki jana wamembatiza jina ‘Messi’, wakimfananisha Mwanasoka Bora wa Ulaya, Muargentina Lionel Messi.
    Ngassa jana amewalamba vyenga wacheaji wa Bidvest Wits na kumpasia Danny Venter kufunga bao pekee dakika ya 72 Free State Stars ikishinda 1-0 na kutinga Robo Fainali za michuano ya Kombe la Telkom Knockout Afrika Kusini.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Goble Park mjini Bathelehem yalipo makao makuu ya Free State, Ngassa alicheza soka ya nguvu kiasi cha mashabiki kumuimba ‘Messi Messi’ kila anapokuwa na mpira.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo, Ngassa amesema sasa anafurahia maisha Afrika Kusini na jana mashabiki wamempa jina Messi.
    “Baada ya mechi viongozi wa Bidvest walinifuata na kuchukua namba yangu, wanaonyesha nia ya kunihitaji. Kwa kweli sasa ninacheza na watu sasa wanajua kuna mtu anaitwa Ngassa,”amesema.
    Ngassa anapanda ndege mchana wa leo kurejea Dar es Salaama mara moja kujiunga na kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars kwa maandalizi ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Malawi.
    Stars: Diakite, Mashego, Sankara, Chakoroma/Mohomi dk28’, Rakoti, Thlone, Ngasa, Masehe, Venter, Fileccia na Ngcobo/Sekola dk46.
    Wits: Josephs, Allie, Hlatshwayo, Mkhwanazi, Bhasera, Pelembe/Motshwari dk80, Shongwe, Ntshangase, Klate, Vilakazi/Kadi dk61 na Lupeta/Mahlambi dk60.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA AJENGA HESHIMA ‘SAUZI’, AFANYA MAMBO BALAA FREE STATE YASHINDA 1-0, BIDVEST WITS ‘WAKOLEA’ KWA MRISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top