• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2023

  NI YANGA NA RIVERS UNITED ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC watamenyana na Rivers United ya Nigeria katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, wakianzia ugenini na kumalizia nyumbani.
  Hayo ni marudio ni mechi ya Hatua ya 32 Bora msimu uliopita, ambao Yanga ilitolewa na Rivers United kwa jumla ya mabao 2-0 ikifungwa 1-0 nyumbani na ugenini.
  Mechi nyingine za Robo Fainali ni; Pyramids ya Misri dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, US Monastirienne ya Tunisia dhidi ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast na USM Algier ya Algeria dhidi ya FAR Rabat ya Morocco.
  Mechi za kwanza za Robo Fainali zitachezwa Aprili 23 na za marudiano zitafuatia Aprili 30 na Yanga ikivuka hapo itakutana na mshindi kati ya Pyramids na Marumo Gallants.
  RATIBA KAMILI ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO 
  Pyramids         v     Marumo Gallants
  US Monastir    v     ASEC Mimosa 
  USM Algier      v     FAR Rabat 
  Rivers United   v     Yanga SC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI YANGA NA RIVERS UNITED ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top