• HABARI MPYA

  Thursday, April 06, 2023

  FOUNTAIN GATE YATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA SEKONDARI AFRIKA


  TIMU ya wasichana ya Fountain Gate Secondary School ya Dodoma imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya shule za sekondari Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya ushindi wa 2-0 leo dhidi ya Scan Aid ya Gambia katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini.
  Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Zainabu Karuka na Winfrida Hubert na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita na kuongoza Kundi baada ya kushinda 7-1 jana dhidi ya wenyeji, Edendale Technical School.
  Taasisi ya Motsepe Foundation, inayomilikiwa n Rais wa CAF imechangia dola za Kimarekani Milioni 10 kwenye michuano hiyo na kuifanya iwe ya kitajiri Zaidi miongoni mwa michezo ya wanafunzi barani. 
  Mshindi kwa upande wa wasichana na wavulana atazawadiwa USD 300,000 kila mmoja na washindi wa pili watapata USD 200,000 wakati wa tatu atapata USD 150,000.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YATINGA NUSU FAINALI MICHUANO YA SEKONDARI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top