• HABARI MPYA

  Friday, September 02, 2022

  MUUZA DUKA ASHINDA MAMILIONI YA M-BET


  MKAZI wa Dar es Salaam Raphael Daudi amejishindia kitita cha Sh 113,789, 620 baada ya kubashiri kiusahihi mechi 12 za mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.
  Daudi ambaye ni muuza duka eneo la Ubungo Riverside na shabiki wa Simba alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa yeye kushinda kiasi kikubwa cha fedha hicho kutokana na ugumu wa kubashiri kwa baadhi ya timu zilizokuwa zinacheza.
  Alisema kuwa mchezo kati ya Crystal Palace dhidi ya Brentford FC ulimpa ugumu sana kubashiri kwa uharaka kutokana na matokeo ya timu zote mbili kabla ya mchezo huo.
  “Mchezo huo ulikuwa mgumu sana kwangu kutabiri kutokana na matokeo ya awali, nilishindwa kubashiri haraka na baada ya kufikiria sana, nilibashiri matokeo ya sare na ndivyo ilivyokuwa,”alisema Daudi.
  Daudi ambaye pia ni shabiki wa klabu ya Simba alisema  kuwa atazitumia fedha hizo kwa kuongeza mtaji katika biashara zake na nyingine kujiendeleza kimasomo.
  Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema Daudi anakuwa mshindi wa nane wa mwaka huu kuibuka mshindi katika jackpot ya PERFECT 12  tokea kuanza kwa mwaka huu.
  Mushi pia aliwaomba Watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiri kupitia M-BET ili waweze kubadili maisha na kushinda mamilioni ya fedha.
  Mkuu wa Kitengo Cha Wateja Binafsi wa Benki CRDB, Stephen Adili alimpongeza Daudi kwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha na kumshauri kutumia kiasi hicho cha fedha kuwekeza.
  “Nampongeza Daudi kwa ushindi huu mkubwa na kikubwa zaidi ni mteja wa benki yetu yenye ushirikiano mkubwa na kampuni ya M-Bet Tanzania. Nawaomba vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na M-BET na vile vile kuweka fedha zao katika benki yetu na kuweza kushiriki katika promosheni yetu maarufu ya kuelekea kombe la dunia nchini Qatar,” alisema Adili.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  Unknown said... September 19, 2022 at 4:59 PM

  Mbona jana nime shinda lakini hela haikuingiav

  Item Reviewed: MUUZA DUKA ASHINDA MAMILIONI YA M-BET Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top