• HABARI MPYA

  Friday, September 02, 2022

  MAN UNITED YASHINDA MECHI YA TATU MFULULIZO


  TIMU ya Manchester United imepata ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa King Power, Leicester, Leicestershire.
  Bao pekee la Man United jana limefungwa na Jadon Sancho dakika ya 23 akimalizia pasi ya Muingereza mwenzake, Marcus Rashford.
  Huo unakuwa ushindi wa tatu mfululizo chini ya kocha mpya, Mholanzi Erik ten Hag baada ya mwanzo mbaya wakipoteza mechi mbili mfululizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YASHINDA MECHI YA TATU MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top