• HABARI MPYA

  Sunday, September 04, 2022

  HAALAND AFUNGA MAN CITY YATOA DROO


  MABINGWA watetezi, Manchester City jana wamelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Man City walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake mpya, Mnorway Erling Haaland dakika ya 49, kabla ya mshambuliaji Mjamaica, Leon Bailey kuisawazishia Aston Villa dakika ya 74.
  Man City inafikisha pointi 14 katika mchezo wa sita na inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Arsenal yenye mechi moja mkononi ambayo leo inaweza kuongoza kwa pointi nne iwapo itaifunga Manchester United.
    

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND AFUNGA MAN CITY YATOA DROO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top