• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 01, 2020

  RUVU SHOOTING YAICHAPA COASTAL UNION 3-1 UHURU, KAGERA SUGAR YAILAMBA MTIBWA SUGAR 2-1 KAITABA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Ruvu Shooting leo yamefungwa na nyota wake, Mohammed Issa ‘Banka’ dakika ya 15, Fully Zulu Maganga dakika ya 40 na Eradius Emmanuel dakika ya 81, baada ya Coastal Union kutangulia kwa bao la Raizin Hafidh dakika ya pili.
  Kwa ushindi huo, Coastal Union inayofundishwa na kocha mkongwe, Charles Boniface Mkwasa inafikisha pointi 15 baada ya kucheza mechi tisa na kusogea nafasi ya tano, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC na Biashara United wenye pointi 16 kila mmoja.


  Coastal Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda inabaki na pointi zake tisa baada ya kucheza mechi tisa, sasa ikiwa nafasi ya 13. 
  Nayo Kagera Sugar ikaibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 67 na Yussuph Mhilu dakika ya 69 baada ya Mtibwa Sugar kutangulia kwa bao la Awadh Juma dakika ya 43.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inayofundishwa na Mecky Mexime Kianga inafikisha pointi  nane baada ya kucheza mechi tisa, ingawa inabaki nafasi ya sita, wakati Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Vincent Barnabas inabaki na pointi zake 11 katika nafasi ya 11 baada ya mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YAICHAPA COASTAL UNION 3-1 UHURU, KAGERA SUGAR YAILAMBA MTIBWA SUGAR 2-1 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top