• HABARI MPYA

    Saturday, December 07, 2019

    MTANZANIA AMCHAPA MZUNGU AUSTRALIA, WENGINE WAWILI ULINGO MMOJA NA RUIZ, JOSHUA LEO SAUDIA

    Na Mwandsh Wetu, SYDNEY
    BONDIA Mtanzania, Bruno Melkory Tarimo ‘Vifua Viwili’ (pichani kushoto) jana amefanikiwa kutwaa taji la IBF International uzito wa Super Feather baada ya kumshinda kwa pointi mwenyeji, Nathaniel May ukumbi wa ICC Exhibition Centre mjini Sydney, Australia.
    Bondia huyo mzaliwa wa Rombo, mkoani Kilimanjaro mkazi wa Bagamoyo, mkoani Pwani alimzidi kwa kiasi kikubwa mpinzani wake huyo kwenye pambano hilo la raundi 10 na haikuwa ajabu kutangazwa mshindi jana. 
    Hilo linakuwa pambano la 28 kwa Tarimo tangu ajiunge na ngumi za kulipwa Desemba 25, mwaka 2013 akiwa ameshinda mara 25, mara tano kwa Knockouts (KO), amepigwa mara mbili zote kwa KO na droo moja.  
    Wakat huo huo, mabondia wengine wawili wa Tanzana watapigana leo katika mapambano ya utangulizi kabla ya Mmarekani mwenye asili ya Mexico, Andy Ruiz Jr. kuzipiga na Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Anthony Joshua ukumbi wa Diriyah Arena mjini Diriyah nchini Saudi Arabia.
    Hilo litakuwa pambano la marudiano baada ya Juni 1, mwaka huu Joshua kupigwa kwa KO raundi ya saba na kupokonywa mataji ya WBA, IBF, WBO na IBO, tena akikalishwa mara nne. 
    Mtanzania Swedi Mohamed atapigana na Ivan 'Hopey' Price wa Uingereza katika uzito wa Super Bantam na Suleiman Said atachapana na Mmarekani Diego Pacheco katika uzito wa Middle.
    Mapambano mengine ya utangulizi leo Alexander Povetkin atachapana na Michael Hunter, Filip Hrgovic na Eric Molina, Dillian Whyte na Mariusz Wach na Mahammadrasul Majidov dhidi ya Tom Little, yote uzito wa Heavy.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTANZANIA AMCHAPA MZUNGU AUSTRALIA, WENGINE WAWILI ULINGO MMOJA NA RUIZ, JOSHUA LEO SAUDIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top