• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 01, 2019

  AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA JKT TANZANIA LEO KATIKA LIGI KUU CHAMAZI

  Mwandishi Wetu, DARES SALAAM
  TIMU ya Azam FC leo imeshindwa kutumia vyema fursa ya kucheza nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na  JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Kwa sare hiyo, Azam FC inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 10 wakati JKT Tanzania inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 13.  
  Azam FC inayofundishwa na kocha Mromania, Aristica Cioaba leo ilikuwa ina kazi ya kusawazisha tu mabao baada ya kutanguliwa na JKT mara zote.


  Mshambuliaji Edward Songo alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya 14 bao ambalo lilidumu hadi dakika ya 79 beki, Aggrey Morris alipoisawazishia Azam Fc kwa penalti dakika ya 79. 
  Mshambuliaji wa zamani wa Coastal Union, Simba na Singida United, Daniel Lyanga akaiadhibu timu yake nyingine ya zamani kwa kuifungia JKT Tanzania bao la lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 86, kabla ya chipukizi Iddi Suleiman kuisawazishia Azam FC dakika ya 88.
  Ligi Kuu ya Tanzania Bara itaendelea kesho kwa mchezo mmoja tu, Yanga SC wakimenyana na KMC Uwanja wa Uhuru Jiji Dar es Salaam.
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Mudathir Yahya/Iddi Kipagwile dk75, Iddi Suleiman ‘Nado’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Obrey Chirwa, Shaaban Iddi Chilunda/Donald Ngoma dk46 na Joseph Mahundi/Salmin Hoza dk46.
  JKT Tanzania; Patrick Muntary, Damas Makwaya, Adeyum Ahmed, Frank Nchimbi, Rahim Juma, Jabir Aziz, Mwinyi Kazimoto, Richard Maranya, Daniel Lyanga, Adam Adam/Mohamed Rashid dk85 na Edward Songo/Mohamed Fakhi dk90.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA JKT TANZANIA LEO KATIKA LIGI KUU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top