• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 01, 2019

  SAMATTA AFUNGA BAO LA KUONGOZA LAKINI KRC GENK YACHAPWA 2-1 NYUMBANI LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana aliifungia bao la kuongoza timu yake, KRC Genk ikichapwa 2-1 na Sint-Truiden katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alifunga bao hilo dakika ya tisa tu akimalizia kazi nzuri ya kiungo Mromani, Ianis Hagi kabla ya wenyeji kuzinduka kwa mabao ya washambuliaji wake, Mfaransa Yohan Boli dakika ya 18 na Mjapan Yuma Suzuki dakika ya 41.
  Kipigo hicho kinaifanya Genk ibaki na pointi zake 21 baada ya kucheza mechi 16 na sasa inazidiwia pointi 18 na vinara, Club Brugge huku ikiwa inalingana na Sint-Truiden.

  Bao hilo linamfanya Samatta afikishe jumla ya mabao 71 katika mechi 177 za mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 138 akiwa amefunga mabao 54, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya mabao matau, mechi nne.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Coucke, Maehle, Cuesta, Lucumi, De Norre/Ndongala dk81, Piotrowksi/Onuachu dk61, Berge, Hagi, Samatta na Bongonda/Paintsil dk61.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA BAO LA KUONGOZA LAKINI KRC GENK YACHAPWA 2-1 NYUMBANI LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top